Mtoto wa aliyekuwa mtabiri bingwa, Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan Hussein ametabibiri kuwa Katiba Mpya itapatikana kwa mbinde, kwani kutakuwa na malumbano na utata hasa kuhusu ajenda ya Serikali tatu.
Katika utabiri wake pia amesema kuna kiongozi
mmoja wa chama cha siasa nchini ambaye atandolewa kwenye uongozi na
kitendo hicho kinaweza kumsababishia anguko la kisiasa kwake au hata
kifo.
Alisema hali kadhalika, kiongozi mmoja wa kisiasa
mwenye wafuasi wengi na umaarufu mkubwa, mwishoni mwa mwaka huu ataugua
kichaa na kumsababishia kuanguka kisiasa. Hussein alisema mbali na hayo,
Tanzania itakumbwa na msiba wa kitaifa huku umaarufu wa Rais Jakaya
Kikwete, ukizidi kuongezeka hasa kwa kutatua migogoro mikubwa nchini.
Alisema Rais Kikwete pia atafanya tukio kubwa la kutikisa nchi, lakini tukio hilo litaleta neema.
“Uadui wa taasisi au chama utakuwa mkubwa na kuna
dalili za kupigana kwa wafuasi wa vyama pinzani, Tanzania itaingia
kwenye mzozo na nchi jirani na wanasiasa wataendelea kukumbwa na kashfa
za ngono,” alisema.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, Maalim Hussein alisema, “Mwaka huu umenzia siku ya Jumatano na
unaashiria shida, maradhi na vifo kwa watu maarufu wakiwemo wasanii na
wanahabari.”
Alisema katika mambo ambayo ameyatabiri ni vyema
Serikali ikawa makini kwani mwaka huu kuna majanga mengi ambayo yatatoke
hasa vifo, shida na maradhi.
Alisisitiza kuwa kwa upande wanasiasa na viongozi
wa dini watafariki, pia wasanii, wanahabari na wanasiasa. Hivyo ni vyema
wakawa makini kwa mambo wanayoyafanya.
“Mwaka huu unaonyesha kuwa kutakuwa na neema kwa
vijana hasa wasanii, wanahabari, lakini kwa upande wa vifo inaonyesha
watakufa wengi, ni vyema wakawa makini,” alisema Maalim Hussein.
No comments:
Post a Comment