Waswahili husema; matatizo hayapigi hodi. Ndivyo ilivyo siyo kwa waswahili tu, bali kwa binadamu wote.
Miongoni mwa watu wanaoweza kuelezea vyema kauli hiyo msichana Delfina Cedeno (19), ambaye hutokwa na machozi na jasho la damu.
Ugonjwa huo unaotajwa na madaktari kama siyo wa
kawaida, pia umemfanya Cedeno kutoka damu kwenye kucha na kitovu kwa
muda wa miaka minne sasa.
Hali ya binti huyo ambaye alianza kupoteza
matumaini ya kuishi, ilizidi kuwa mbaya baada ya kuanza kutokwa na damu
puani, huku nywele zake zikinyofoka kila siku.
Akizungumza na gazeti la Mirror, Delfina, ambaye
ni mkazi wa Veron, Jamuhuri ya Dominica, anasema kuwa wakati Fulani,
aliwahi kutokwa na damu kwa muda wa siku 15 mfululizo, hata kulazimika
kuongezewa dripu za damu.
Vipimo alivyofanyiwa
Anasema kuwa hadi sasa ameshafanyiwa vipimo zaidi
ya mia moja, lakini hakuna daktari hata mmoja aliyeweza kubaini chanzo
cha tatizo lake.
“Wakati tatizo hili linaanza kunitokea sikujua nifikiri nini, niliogopa na kubaki na mshituko mkubwa.
Mwanzoni hakuna mtu aliyetaka kunisaidia, walikuwa
wananiangalia kama vile mimi ni kichaa pale nilipojaribu kuwaambia kitu
gani kinanitokea,” anasimulia Delfina na kuongeza:
“Hadi pale siku moja nilipoanza kutokwa na damu mbele ya daktari, ndipo walipoanza kulipa umuhimu suala langu.”
Anasema kuwa kutokana na hali yake, anajisikia
vibaya hadi kushindwa kuendelea kuishi nyumba moja na mama yake
anayejulikana kwa jina la Mariana.
Delfina alilazimika pia kuacha masomo, baada ya rafiki zake wengi kuadhani kuwa huenda angewaambukiza ugonjwa aliokuwa nao
Anasema: “Watu waliniogopa. Walidhani kama wakinishika
ningewapaka damu. Watoto wananicheka na kunipigia kelele, muda mwingi
ninashinda chumbani kwangu.”
Baada ya kukata tamaa ya kuishi, siku moja binti
huyo aliamua kunywa kiwango kikubwa cha dawa ili ajiue, lakini madaktari
walifanikiwa kumwokoa.
Anasema: “Nilitaka kufa. Familia yangu ilinikuta
nikiwa na hali mbaya chumbani kwangu, huku nikitoka povu mdomoni.
Niliishia kukaa chumba cha uangalizi maalumu kwa muda wa wiki nzima hadi
nilipozinduka. Ni kama vile nilikuwa nimekufa.”
Anaongeza: “Nilizidiwa, nikawa ninapigwa kwa shoti
ya umeme. Kwa kweli kulikuwa na uwezekano ningevunjika mbavu zangu.
Lakini inashangaza kwamba sasa ni mzima. Nina furaha kwa sababu maisha
yangu yameanza kuimarika.”
Siku moja akiwa hospitali, alitembelewa na
mwanaume mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Recaris Avila, ambaye baadaye
alikuja kuwa rafiki yake wa kiume.
“Aliniambia mimi ni mzuri. Nitaikumbuka hiyo siku zote za maisha yangu,”anasema.
Baada ya miaka minne ya mateso, hatimaye madaktari wameanza kuelekea kupata tiba ya ugonjwa wake.
Wanasema kuwa Delfina unasumbuliwa na ugonjwa
unaoitwa Hematidrosis, unaomaanisha kwamba ana kiwango kikubwa cha
adrenaline kinachofikia mara 20 ya mtu wa kawaida.
Chanzo chake
Ugonjwa huo humpata mtu anapokuwa na kiwango
kikubwa cha hofu, hivyo kufanya shinikizo la damu kuwa juu na kumfanya
atoke jasho la damu.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la
India la Dermatology, mishipa mingi ya damu inayozunguka sehemu za
kutolea jasho hubana na kuwa na wembamba wakati mtu anapokuwa na
shinikizo la damu.
Hofu inapoongezeka, mishipa ya damu hupasuka. Damu
huingia hupita kwenye matundu ya jasho na hivyo kutengeneza
mchanganyiko wa damu na jasho.
Madaktari wamempa Delfina dawa ya kudhibiti hofu ambayo imemsaidia kupunguza damu kutoka mwilini.
Akimsifu mchumba wake ambaye wameahidiana kufunga
ndoa, Delfina anasema: “Namshukuru Recaris maana ninajisikia nipo huru
na sitaki tena kufa. Kukutana naye lilikuwa jambo la furaha sana. Bado
ninaweza kuanza kutoka tena damu, lakini sina wasiwasi kwa kuwa najua
yupo karibu yangu kunisaidia.”
Kwa upande wake Avila anasema: “Ninauona urafiki
wetu ni wa kawaida pamoja na hali aliyonayo, nampenda. Kwangu yeye ni wa
kawaida, ingawa wakati mwingine anajisikia vibaya kwa sababu hataki
mimi nimwone akitoka damu.
“Mimi namwambia sina wasiwasi, nina furaha
No comments:
Post a Comment