Watoto wadogo walibebwa au kusimama kwenye mabega ya watu wazima, huku chumba kikiwa kimejaa maji. Hii ni hali ambayo ilitokea katika mafuriko ya hivi karibuni yaliyotokea Kilosa, mkoani Morogoro.
Hali ya mambo
Ilikuwa siku yenye mateso makubwa na uchungu wa
kupotelewa na mali mbalimbali kwa wananchi wa Kijiji cha Magole, ambao
walizingirwa na mafuriko.
Kila mtu alikuwa na aina yake ya kujiokoa; wapo
niliowaona wakiwa juu ya miti ilimradi tu ni namna gani ya kutafuta
njia ya kujinusuru na kifo.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Magole Wilaya ya
Kilosa Mkoa wa Morogoro, Marthin Kongera (42) anaeleza mkasa mzima
uliyoikumba familia yake pamoja na yeye mwenyewe na majirani
waliokimbilia katika nyumba yake iliyojengwa na matofali ya saruji yenye
vyumba viwili na ukumbi mmoja ili kuweza kujihifadhi na mafuriko
yaliyoikumba tarafa ya Magole Januari 22 mwaka huu saa 12 asubuhi.
Akizungumza na mwandishi wa makala haya katika nyumba za Shule ya Msingi Magole, Kongera anasema kuwa ilikuwa siku ya Jumanne, yeye na familia yake waliamka salama saa 12 asubuhi, baada ya muda mfupi akijiandaa kwenda kazini (shule mita 40 tu kutoka nyumbani kwake). Alianza kuona maji yakitiririka huku yakiwa yamesomba uchafu na kadiri muda ulivyozidi kusogea mbele maji yaliendelea kufika eneo la shule na kuanza kusambaa sehemu kubwa.
Maji hayo yalielekea kwa kusambaa kwa kasi katika mitaa ya kijiji hicho.
“Ni miujiza ya
KWA HABARI ZAIDI Mwenyezi Mungu kwani kama hakupenda ufe huwezi kufa. Ndivyo ilivyotokea kwetu sisi, kama Mungu angependa tufe katika mafuriko haya basi katika nyumba yangu wangeopoa maiti 25 ya watu wazima na watoto,” anasema Kongera.
KWA HABARI ZAIDI Mwenyezi Mungu kwani kama hakupenda ufe huwezi kufa. Ndivyo ilivyotokea kwetu sisi, kama Mungu angependa tufe katika mafuriko haya basi katika nyumba yangu wangeopoa maiti 25 ya watu wazima na watoto,” anasema Kongera.
Baada ya familia ya mwalimu huyo kuzingirwa na
maji hayo walishindwa kuyakimbia hasa baada ya maji mengine zaidi
kuwavamia katika eneo hilo walilokuwepo.
Wakati akiangalia namna ya kujiokoa, kundi la
majirani nalo liliingia kwenye nyumba yake kuomba msaada wakifikiri
kwamba kwa vile nyumbani hiyo ni ya tofali maji yasingeweza kuathiri
kama ilivyo kwao; kwani walitoka kwenye nyumba zilizojengwa kwa udongo
na kuezekwa kwa nyasi, siyo tofali na bati kama ilivyo nyumba ya
mwalimu.
Kongera anasema baada ya maji kuzidi na hakuna pa kukimbilia yeye pamoja na familia yake na wale majirani zake alichukua uamuzi wa kufunga milango na madirisha kisha kuwaamuru kinamama wasimame juu ya makochi na meza na watoto kusimama juu ya mabega ya mama zao huku wakiwa wameshikilia nondo za madirisha kwa muda wa zaidi ya saa nne.
Anasema kilichowaokoa ni kusaidiwa na watu. Lakini kilichowaokoa
zaidi ni kupungua kwa maji kufuatia Serikali kubomoa sehemu ya barabara
na kuruhusu maji yaliyotuama kwa saa kadhaa kupungua na kuwapa afueni
wao na wananchi wengine waliokuwa wamepanda juu ya miti, mapaa ya nyumba
na juu ya dari za nyumba kujikoa.
Siku ya tukio baadhi ya wananchi walioathirika
zaidi na mafuriko hayo walishinikiza uongozi wa Serikali ya kijiji kutoa
ruksa ya vijana kubomoa sehemu ya barabara hiyo ili kutoa nafasi ya
maji yaliyotuama kupungua ili watu walioshindikana kuokolewa hasa wale
waliopanda juu ya miti, paa za nyumba na dari za nyumba waweze kujiokoa.
Baadhi ya watu walikuwa wakisikika wakiomba msaada lakini walishindwa
kuwaokoa kutokana na waogeleaji kuwa wachache.
Fatuma Abdallah Funge (62) anaelezea namna alivyojiokoa katika mafuriko hayo kuwa bila msaada wa vijana angepoteza maisha.
“Nawashuru vijana wawili ambao waliogelea na
kufanikiwa kunibeba ili kunipeleka nchi kavu lakini juhudi zao
zilishindikana baada ya wenyewe kuchoka na kuamua kunipandisha juu ya
mti eneo la Shule ya Msingi Magole hapo ndipo palikuwa na kazi kubwa ya
kunipandisha,” anasema Fatuma.
Aliongeza kuwa alisikia karaha sana wakati
akipandishwa juu ya mti, hali hiyo ilitokana na yeye kushindwa kupanda
kwani ni mzee, hivyo mmoja alitangulia juu ya mti huo na kumshika mkono
na mwingine aliyesimama chini kumshika mwili na kufanikiwa kumpandisha
juu.
Wakati akiwa kule juu mti, alipatwa na baridi kali
na mwili mzima kuuma na baada ya maji hayo ya mafuriko kupungua, vijana
hao walimshusha.
“Niliwaona watu wengine zaidi ya 30 wakiwa
wamepanda juu ya miti. Nashukuru kuwa miti hii imekuwa mwokozi katika
mafuriko haya,” anasema bibi huyo.
Mbali ya wananchi kupoteza mali katika janga hilo,
ofisi ikiwemo shule, mahakama na ofisi za kijiji na kata ni miongoni
mwa walioathiriwa kwa kusombwa na maji, huku baadhi yake zikiharibiwa
kwa maji hayo yaliyojaa kila aina ya uchafu.
Mkazi wa kijiji hicho Shida Abdallah (24)
anakumbuka namna alivyonusurika kifo kwa kusombwa na maji ya mafuriko
kwa umbali wa mita 350 kabla ya kufanikiwa kuparamia mti na kukaa juu
yake kwa zaidi ya saa 12 kabla ya kuokolewa. Akiuzungumzia mkasa huo,
Abdallah anasema akiwa shambani akilinda mazao yake yakiwamo miwa,
mahindi na minazi; akiwa amelala usiku wa Januari 21 saa 8 usiku
alishtushwa na ubaridi wa maji mwilini mwake
No comments:
Post a Comment