Kiongozi wa waasi wa Jamhuri ya Kati Paul Joseph Mukungubila ameikosoa Serikali ya nchi hiyo na kumtaka Rais Joseph Kabila aondoke madarakani.
Kauli hiyo ni baada ya shambulio ambalo
lilifanyika mwishoni mwa Desemba ambapo watu waliokuwa na silaha
walishambulia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ndjili, kambi ya jeshi na
kituo cha redio na televisheni ya Serikali.
Baada ya uvamizi huo Rais Joseph Kabila wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo alitoa wito kwa wananchi akiwataka waimarishe
mapambano ya pande zote.
Kwa upande wake msemaji wa Serikali Lamberte Mende
Omalanga alitangaza kuwa watu hao ni magaidi waliotaka kuzusha wasiwasi
na woga kwa wakazi wa Kinshasa kabla ya kuanza mwaka mpya.
Watu hao wanaotajwa kuwa ni wafuasi wa kiongozi wa
kidini Paul Joseph Mukungubila, walipigana pia na askari usalama katika
miji ya Kindu na Lubumbashi, lakini askari walifanikiwa kuwashinda
waasi hao na kudhibiti miji hiyo.
Hata hivyo ujumbe uliotolewa Desemba 30 na Joseph
Mukungubila kwa Wakongo ulionyesha kuwa mashambulizi hayo yalikuwa
jaribio la mapinduzi.
Mukungubila alisema katika ujumbe huo kwamba lengo
lake ni kuwakomboa Wakongo kutoka katika kile alichodai kuwa ni ‘utumwa
wa Rwanda’.
Wanadiplomasia mbalimbali wanaamini kuwa,
kuashiriwa utumwa wa Rwanda kunatokana na ukweli kuwa Laurent Kabila,
baba wa Rais wa sasa wa Kongo aliyepindua Serikali ya dikteta Mobutu
Seseko wa Zaire ya wakati huo, alikuwa akiungwa mkono na Rwanda.
Baada ya kuanguka utawala wa Mobutu Seseseko,
Laurent Kabila ambaye alikuwa akisaidiwa na marais wa wakati huo wa
Rwanda na Uganda, aliingia madarakani nchini Zaire na kubadilisha jina
la nchi hiyo kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Hata hivyo, baada ya Laurent Kabila kushindwa
kudhamini masilahi ya majirani wa Kongo na Marekani katika eneo la
Maziwa Mkuu ya Afrika, waitifaki wake hao walianzisha vita vipya dhidi
ya Kinshasa.
Vita vya ndani nchini Kongo kati ya mwaka 1998 na
2003 vilianza baada ya wanajeshi wa Rwanda na Uganda kushambulia mipaka
ya nchi hiyo.
Katika vita hivyo Angola, Namibia na Zimbabwe
zilikuwa zikimuunga mkono Laurent Kabila, na baada ya muda mfupi nchi 8
za eneo la Maziwa Makuu barani Afrika zikaingia kwenye vita hivyo, na
ndiyo sababu mapigano hayo yakapewa jina la ‘vita vya kwanza vya dunia
barani Afrika.
No comments:
Post a Comment