Mwenyekiti wa Chama cha Demokratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila anatarajia kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kuendelea kwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba Mpya.
Mchungaji Mtikila akizungumza na gazeti hili
alisema, madhumuni ya kufungua kesi hiyo ni mchakato huo kukiuka hatua
mbalimbali muhimu wakati wa kuiandaa ikiwamo kutoa elimu kwa wananchi
kipi wanatakiwa kukifanya kabla ya kutoa maoni.
“Nakwenda kufungua kesi hiyo, kutaka mchakato huu
unaoendelea ufutwe na utupiliwe mbali, tunataka mchakato
unaowashirikisha Watanzania wote, walio katika vyama vya siasa,makundi
mbalimbali ya kiraia na madhehebu ya dini na wasio na makundi wala
madhehebu,” alisema Mtikila
Aliongeza “Nilikuwa kimya najipanga, najua
nitashinda sijajua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataniletea mawakili
wangapi lakini nitampangua mmoja baada ya mwingine.” Mchungaji Mtikila
alisema, endapo majaji wa mahakama hizo watakaoisimamia kesi hawatatenda
haki kutokana na matakwa ya Serikali ya CCM atakata rufaa.
No comments:
Post a Comment