Taarifa ya waasi wa Sudan
Kusini inasema kuwa mjumbe wa Marekani, Donald Booth, pamoja na
wapatanishi wa kanda ya Afrika Mashariki, wamezungumza na kiongozi wa
waasi hao, Riek Machar.
Taarifa hiyo iliyopokewa na shirika la habari la
Ufaransa ilieleza kuwa mazungumzo hayo yalifanywa Jumamosi lakini
haikutaja yalifanywa wapi.Hakuna mtu mwengine aliyethibitisha habari hizo.
Mazungumzo ya amani nchini Ethiopia ambayo yanalenga kumaliza majuma mane ya vita nchini Sudan Kusini hayaoneshi kuwa yamepiga hatua.
Inaonekana kizuiizi kikubwa ni shuruti ya Bwana Machar kuwa wafuasi wake 11 waachiliwe huru mjini Juba.
No comments:
Post a Comment