Wapalestina wakisherehekea kifo cha Ariel Sharon
Watu nchini Israel
leo wanaanza kipindi kifupi cha maombolezi kufuatia kifo cha waziri
mkuu wa zamani Ariel Sharon aliyefariki akiwa na umri wa miaka 85 baada
ya miaka 8 ya kuwa hali mahututi.
Wananchi watatoa heshima zao za mwisho kwa mwili wake Jumapili kabla ya kuzikwa Jumatatu.Lakini aliwaacha wapalestina wengi waliomuona kama adui wao wakiwa na hamaki.
Mkuu wa kituo cha afya cha Sheba mjini Tel Aviv alithibitisha kifo cha Sharon, Jumamosi mchana siku ya Sabato kwa wayahudi, zaidi ya wiki moja baada ya taarifa kutolewa kuhusu afya yake kuzorota.
Mmoja wa wanawe Sharon,Sharon, Gilad Sharon, alisema kuwa babake amekwenda wakati alipoamua mwenyewe kwenda.
Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama, wamesema Sharon, alikuwa kiongozi aliyejitolea kuwahudumia watu wa Israel.
Rais Shimon Peres, mwandani mkuu wa Sharon japo alikuwa hasimu wake wa kisiasa aliyejiunga na serikali ya Muungano na Sharon mwaka 2001, alisema Sharon alikuwa mtu mwema aliyepigania watu wake na kuwapenda na kuwa watu pia walimpenda.
Wadhifa wa Sharon kama waziri mkuu ulifika kikomo baada ya kupatwa na kiharusi na kisha kuwa katika hali mahututi kwa miaka minane tangu mwaka 2006.
Wakati huu wote alikuwa anatumia mashine kupumua na mirija kulishwa chakula.
Kabla ya hali ya Sharon kuzorota aliongoza jeshi la Israel kuondoka katika ukanda wa Gaza ili kupunguza taharuki kati ya Israel na Palestina.
No comments:
Post a Comment