Blogger Widgets

Friday, 26 July 2013

DAVID MOYES; "MAZUNGUMZO YANAENDELEA KATI YETU NA BARCELONA KUHUSU FABREGAS"


DAVID MOYES amethibitisha kwamba Manchester United bado wapo kwenye mazungumzo na Barcelona juu ya usajili wa Cesc Fabregas.

United wameshatuma ofa mbili kwa ajili ya kiungo wa zamani wa Arsenal kwenye dirisha hili la usajili.

Alipoulizwa kama kuna maendeleo yoyote juu ya usajili wa Fabregas, Moyes alijibu: “Mazungumzo ya mtu yanaendelea.”
Moyes pia alitoa taarifa kwamba Robin van Persie anaendelea vizuri na yupo fiti kucheza mechi ya kesho dhidi ya Cerezo Osaka.

Wakati huo huo pia, kocha huyo wa Scotland amesisitiza anataka kuendelea kuwa na makinda yenye vipaji vikubwa Adnan Januzaj na Jesse Lingard kwenye klabu yake kuliko kuwatoa kwa mkopo. 

Moyes alisema: “Wote wawili wamefanya kazi nzuri. Wamezoea vizuri kucheza kikosi cha kwanza na wametoa mchango mkubwa kwenye timu..
“Nina matumaini kwamba tutaweza kuwa nao wote na kuwapa nafasi ya kucheza msimu ujao lakini wote wawili wanahitaji kuendeleza jitihada zao na kuimarisha viwango vyao.”

No comments:

- See more at: http://www.helperblogger.com/2012/06/jquery-facebook-like-box-popup-with.html#sthash.AGJhd6Gy.dpuf