Blogger Widgets

Saturday, 20 July 2013

ANGALIA AJALI MBAYA YA GARI:KICHWA CHA MWANAMKE CHANASA KWENYE KIOO:



Wakimtoa Dereva kwanza
Wakianza kumuokoa yeye

Hatimaye ameokolewa


Mwanamke mmoja raia wa China amenusurika kifo baada ya gari aliliokuwa amepanda kupata ajali mbaya iliyomsababishia yeye kunasa kakita kioo cha Mbele maeneo ya Jimbo la Guanxi, Mwanamke huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika alikuwa kashapoteza fahamu huku damu nyingi zikimtoka katika kioo hicho.


Juhudi za ziada zilifanywa na askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji kwa kukitanua kioo hicho kwa ustaadi mkubwa huku wakihakikisha hawamkati zaidi mwanamke huyo.


Jambo la kushangaza ni kwamba waokoaji hao walianza kumtoa mwanaume ambaye alikuwa anaenda gari hilo kwanza ili kubaki na mwanamke huyo peke yake, baada ya kufanikiwa kumtoa waliwakimbiza wote hospitali ndani ya gari la wagonjwa liliokuja eneo la tukio.


Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema ya kwamba gari alilopanda mwanamke huyo lilikuwa katika mwendo kasi kumbe dereva wake alikuwa amelala na ghafla mbele yao kulikuwa na role na ndipo walipoligonga kwa nyuma, kwa kuwa mwanamke huyo hakuwa amevaa mkanda force ya tukio zima ilimfanya anase katika kioo.


Imeelezwa kwamba hali zao zinaendelea vizuri, Ingekuwa Tanzania kwetu sijui ingekuwaje. Tupe maoni yako....

No comments:

- See more at: http://www.helperblogger.com/2012/06/jquery-facebook-like-box-popup-with.html#sthash.AGJhd6Gy.dpuf