
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) leo linafikishwa katika Mahakama Kuu na Kampuni ya MacDonald Live Line Technology likidaiwa fidia baada ya kusitisha mkataba wa kukarabati njia ya umeme kati ya Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Kampuni hiyo ambayo imekuwa ikikarabati na
kusafisha njia za umeme bila kuuzima, imeamua kuchukua hatua hiyo baada
ya Tanesco kuishinda katika usuluhishi wa mgogoro na kusitisha mkataba
huo.
Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud
alipopigiwa simu jana ili kuzungumzia suala hilo, mara kadhaa alijibu
kwa kifupi kuwa alikuwa akiendesha gari hivyo asingeweza kuzungumza na
simu.
Mkurugenzi wa MacDonald Live Line Technology,
Macdonald Mwakamele alisema msuluhishi wa mgogoro huo aliipa ushindi
Tanesco na kuitaka MacDonald kulipa gharama kwa shirika hilo kama fidia
na usumbufu uliotokana na kutokamilisha kazi iliyopewa katika mikoa hiyo
Alisema kampuni hiyo ilipeleka malalamiko yake kwa
msuluhishi, Wakili Mtango Jonathan Lukwalo, baada ya Tanesco kusitisha
mkataba kwa kampuni hiyo kwa madai kuwa ilichelewa kutekeleza kazi ya
ukarabati wa njia za umeme mkoani Arusha.
Mwakamele alisema Tanesco na kampuni hiyo
waliingia mkataba Machi mwaka 2010 wa kufanya ukarabati wa njia ya umeme
njia ya Kilimanjaro-Arusha kwa kutafuta nguzo, kuzisafirisha kwenda
eneo la kazi.
Alisema kazi hiyo ilitakiwa kukamilika ndani ya wiki 32 kuanzia Julai 2010, 28 hadi Machi 9, 2011.
No comments:
Post a Comment