MWAKILISHI pekee katika mashindano ya Big Brother The Chase
kutoka Afrika Mashariki, Feza Kessy, amesema aliingiwa na fikra kwamba
Elikem angekuwa mtu wa karibu yake, kwani waliingia ndani ya nyumba
pamoja lakini mambo yalibadilika ndani ya siku 77 alizoishi humo.
Akizungumza na IK baada ya kutolewa ndani ya jumba
hilo usiku wa juzi Jumapili, Feza alisema haikuwa rahisi kwake kutambua
tabia halisi za Elikem mpaka alipokaa naye kwa muda mrefu ndani ya
jumba hilo.
“Siku naingia ndani ya jumba niliongozana naye,
nilimpenda kwa kumwona tu, lakini yeye bado sana kimapenzi,” alisema
kabla ya IK kumrushia swali ‘Unampenda kweli Oneal?’, “ Ndio” alijibu
Feza kwa sura ya aibu.
Feza alimweleza IK kuwa amekuwa akizozana mara kwa
mara na Oneal kwa kuwa alihisi kwamba Feza alikuwa akimtumia jambo
ambalo halikuwa sahihi.
Baada ya IK kumuuliza iwapo anadhani kuwa Oneal
alikuwa na mwanamke mwingine akimsubiri nje ya jumba hilo, Feza alijibu;
“Sina hakika na hilo.”
IK alipomuonyesha ni nani alimpendekeza kupigiwa
kura za kutolewa, alishtuka baada ya kuona sura ya Dillish ikitokeza,
hata hivyo Feza alisema ameshangazwa na kitendo cha Melvin kumpendekeza
lakini alizungumza naye kabla kwamba alifanya hivyo.
Alipoulizwa anadhani nani atashinda, Feza alisema: “Siwezi kutabiri, lakini Angelo ni mtu ninayemhusudu zaidi.”
Wakati mpenzi wa Feza, Oneal, akitoka wiki
iliyopita alisema: “Kazi niliyowahi kuipenda ndani ya BBA ni ndoa
niliyofunga na Feza, niliifanya kama ndio kweli kwani nampenda sana yule
binti” aliiambia Afrika.
Feza anaondoka ndani ya jumba hilo akiwa zikiwa
zimebaki siku 14 tu mashindano hayo kumalizika, huku akiwa amewaacha
washiriki saba wanaoendelea kuwania kitita cha Dola 300,000 (Sh 480
milioni)
Feza alipata kura nne kutoka Tanzania, Kenya,
Uganda na Botswana. Cleo naye alipata kura nne kutoka Malawi, Afrika
Kusini, Zambia na Zimbabwe huku Dillish akiongoza kwa kupata kura saba
kutoka Angola, Ghana, Ethiophia, Namibia, Nigeria, Sierra Leone na nchi
nyingine za Afrika.
Cleo na Dillish wamefanikiwa kuendelea kubaki
katika mashindano hayo baada ya kupata kura nyingi zaidi kuliko Feza. IK
alifunga shoo kwa kuwataka washiriki waitumie siku ya Jumatatu (jana)
kuwapendekeza wanaostahili kuondoka na wasiangalie urafiki wao.
No comments:
Post a Comment