
Gustavo
aliambiwa wazi na kocha wa Bayern Pep Guardiola kuwa hataweza kupata
nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza hali inayomfanya atafute timu
ya kwenda ambayo itamhakikishia nafasi kwenye kikosi chake.

Endapo
usajili huu utakamilika utakuwa na ahueni kubwa kwa mashabiki wa
Arsenal ambao wamekuwa kwenye huzuni baada ya kumkosa mshambuliaji
Gonzalo Higuain ambaye kwa muda mrefu alidhaniwa kuwa mbioni kujiunga na
Arsenal kabla ya kujiunga na Napoli .
Pamoja na Higuain
Arsenal imeshuhudia ofa zake mbili za kumsajili mshambuliaji Luis Suarez
zikikataliwa na Liverpool ambayo imeshikilia uamuzi wa kutomuuza
mshambuliaji huyo .
Hadi sasa Arsenal imesajili mchezaji mmoja pekee ambaye ni mchezaji wa timu ya vijana ya Ufaransa Yaya Sanogo.
No comments:
Post a Comment