Kikundi cha wanaharakati nchini Uingereza kimeanza
juhudi za kutaka makampuni ya vyakula na vinywaji vya kuhifadhiwa kwenye
chupa na mikebe kama Soda kupunguza kiwango cha sukari katika bidhaa zao.
Hii ni sehemu ya kampeini ya kutaka kukabiliana
na tatizo la kiafya la unene kupita kiasi pamoja na ugonjwa wa kisukari
nchini humo.Kikundi hiki kimeanzishwa na wanaharakati walioanzisha harakati za kushurutisha makampuni kupunguza kiwango cha Chumvi katika vyakula vinavyohifadhiwa kwenye mikebe tangu mwaka 1990.
Wanaharakati hawa wanataka kuwajulisha watu kujizuia na vyakula vyenye sukari nyingi na kushurutisha wenye makampuni kupunguza sukari katika vyakula hivyo.
Aidha wanaharakati wanataka kuiwekea malengo sekta ya chakula kupunguza kiwango cha sukari hatua kwa hatua kiasi cha wateja kukosa kutambua tofauti yoyote katika ladha ya vyakula hivyo.
Sukari ni bidhaa ambayo hutumiwa sana katika vyakula vingi ikiwemo, mikate, soda, vyakula vya mkebe na katika vyakula vingine ambavyo hata havihitaji sukari.
Na ndio maana sio jambo la kushangaza kuwa soda moja ya mkebe ina vijiko saba vya sukari.
Maji, Yoghurt na vyakula vingine ambavyo hata havihitaji kuwa na sukari vinawekwa sukari.
No comments:
Post a Comment