Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina
Maafisa nchini Madagascar wanasema kuwa matokeo ya
mwanzo mwanzo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Rais uliofanyika mwezi
Disemba, yanaonyesha mshindi kuwa waziri wa zamani wa fedha Hery
Rajaonarimampianina.
Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo inasema kuwa bwana
Hery Rajaonarimampianina alishinda asilimia hamsini na tatu ya kura
zilizopigwa.Mshindani wake, Jean Louis Robinson anasema kuwa uchaguzi ulikumbwa na wizi wa kura na sasa anasema sharti shughuli ya kuhesabu kura irejelewe.
Uchaguzi huo ulikuwa mpango wa kurejesha utulivu kwa nchi hiyo baada ya mapinduzi ya kijeshi kufanyika miaka minne iliyopita.
Bwana Rajaonarimampianina alikuwa mgombea aliyeungwa mkono na kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi, Rais wa zamani Andry Rajoelina.
No comments:
Post a Comment