Kashfa hii imetokea wakati Hollande akikabiliwa na kipindi kigumu cha utawala wake
Rais wa Ufaransa François Hollande, ametishia
kuwachukulia hatua za kisheria wahariri wa jarida moja nchini humo
lililochapisha taarifa za uvumi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na
mwanamke mmoja muigizaji Julie Gayet.
Hollande hakukanusha madai hayo lakini alisema
kuwa jarida hilo limekwenda kinyume na maadili ya vyombo vya habari kwa
kuingilia maisha yake binafsi.Bi Gayet mwenye umri wa miaka 41 ni muigizaji msifika wa vipindi vya televisheni.
Duru zinasema kuwa ufichuzi huu umetokea wakati ambapo Hollande anakabiliwa na changamoto kadhaa katika utawala wake, ikiwemo kudorora kwa uchumi jambo ambalo wananchi wanamtarajia kulishuhughulikia.
Inajulikana wazi kuwa bwana Hollande ana mpenzi mmoja tu ambaye ni mwanahabari Valérie Trierweiler.
Hollande pia aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanasiasa mwenzake wa chama cha kisosholidti, Ségolène Royal.
Mwezi Machi mwaka jana aliwasilisha malalamiko yake kwa kiongozi wa mashitaka Jijini Paris, dhidi ya wanablogu na wenye Mitandao ya kijamii kuwa wanaeneza uvumi.
No comments:
Post a Comment