Blogger Widgets

Tuesday, 30 July 2013

WAZAZI WA GARETH BALE WAINGILIA KATI SUALA LA USAJILI WA MTOTO WAO KWENDA MADRID


Wazazi wa mchezaji GARETH BALE wameingilia kati suala la uhamisho wa mtoto wao anayetakiwa na Real Madrid kwa udi na uvumba katika dirisha hili usajili.

Real Madrid inasemekana wametoa ofa ya kiasi cha £81m kwa Tottenham kwa ajili ya kumsaini winga huyo wa kimataifa wa Wales lakini mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amesisitiza mchezaji huyo hauzwi.

Lakini baada ya mchezaji husika kusemekana kwamba anataka kuondoka Spurs na kujiunga na mabingwa wa kihistoria wa ulaya huku Spurs ikiweka ngumu, leo hii wazazi wa mchezaji wameingilia kati suala hili baada ya kuonekana wakiwa kwenye mkutano mzito na mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy.

Kwa mujibu wa shuhuda wa gazeti la The Sun ni kwamba leo wazazi wa Bale walikutana na Levy kwenye ofisi za Spurs zilizopo kwenye viwanja vya mazoezi vya timu hiyo: “Sikuweza kuamini wakati Bale alipowasili kwenye uwanja wa mazoezi na wazazi wake, mungu anajua nini walienda kuongea na Mr Levy.”

Mwenyekiti huyo wa Spurs alikatisha muda wake wa mapumziko na familia yake na kwa haraka amerudi jijini London kwa ajili kushghulikia suala la Bale.

Lakini pia imeripotiwa kwamba Raisi wa Real Madrid Florentino Perez anatarajiwa kukutana na Levy jijini Miami mapema wiki ijayo ili kuzungumza kuhusu sakata hili la usajili wa Bale.
Perez tayari yupo nchini Marekani - mahala ilipo timu yake ikiwa inajiandaa na msimu mpya.

Inaaminika kwamba baada ya Spurs kukataa ofa ya paundi millioni 82, Real wamerudi na ofa inayohusisha kiasi cha £51 pamoja na wachezaji wwili wa Madrid Angel Di Maria na Fabio Coentrao.

Lakini bado vilabu hivyo vinabishana kuhusu thamani halisi ya wachezaji hao wawili wanaowekwa kwenye dili la usajili wa Bale.

No comments:

- See more at: http://www.helperblogger.com/2012/06/jquery-facebook-like-box-popup-with.html#sthash.AGJhd6Gy.dpuf