wananchi, wasomaji pamoja na wauzaji wa rejareja wa jarida la
Rollingstone, wameshangazwa na kuchukizwa na hata kufikia kusema kuwa ni
sawa na kutusiwa na cover jipya la jarida hilo linalotarajiwa kutoka
mwezi wa nane, ambalo limepambwa na sura ya kijana aliesababisha mauaji
ya Boston Marathon, "Dzhokhar Tsarnaev"
cover hiyo yenye picha nzuuri ya mtuhumiwa huyo ilikuwa na maneno haya.
"THE BOMBER, "How a popular, promising student was failed by his family, fell into radical Islam and became a monster.
malalamiko
ya kitendo cha jarida hilo kumpamba muuaji huyo wa mabomu ya boston
ambayo yaliua watu watatu, kujeruhi zaidi ya 200 pamoja na ofisa wa
polisi mmoja, yalianza kusambaa kupitia mitandao ya kijamii, facebook
pamoja na twitter.
Baada
ya malalamiko hayo kuenea, maduka maarufu yanayouza majarida hayo
yametangaza kugoma kuuza jarida hilo, duka la madawa nchini marekani
CVS limetangaza mgomo wa kutokuweka jarida hilo kwa ajili ya kuuza na
kuungwa mkono na makampuni mengine makubwa kama Walgreens, duka la
glosaries lililopo New England "Stop and Shop", pamoja na Tadesch food
shop
kikubwa
kinacholalamikiwa ni cover hiyo kuwa na picha ya muuaji wa mabomu, na
picha kumuonyesha kama ni innocent na kudai kuwa hakustahili kuwa kwenye
cover ya jarida hilo.
licha
ya malalaniko hayo, wako waliounga mkono gazeti hilo na kusema kuwa,
picha haimaanishi itamfanya muuaji awe ni mtu mzuri, bali
kilichoandikwa, na kilichaandikwa na RollingStone ni maisha aliyokuwa
akiishi kijana huyo na kilichompelekea mpaka kuwa monster, kitu ambacho
ni kizuri kwa watu kuelewa na ni kazi kubwa iliyofanywa na jarida hilo
kupata information zote hizo.
No comments:
Post a Comment