Blogger Widgets
Showing posts with label sports. Show all posts
Showing posts with label sports. Show all posts

Sunday, 2 February 2014

MATOKEO YA JUMAPILI LIGI KUU ENGLAND



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
  • Newcastle         0 - 3         Sunderland 
  • West Ham         2 - 0         Swansea 
  • Cardiff              2 - 1         Norwich 
  • Everton             2 - 1        Aston Villa 
  • Fulham             0 - 3         Southampton 
  • Hull                  1 - 1        Tottenham 
  • Stoke                2 - 1        Man Utd

Wednesday, 29 January 2014

Bingwa wa formular 1 bado mahututi

Mwezi mmoja baada ya kujeruhiwa katika ajali ya mchezo wa kuteleza kwenye barafu, meneja wa jogoo wa mashindano ya mbio za magari ya langalanga, mjerumani Michael Schumacher ameiambia BBC kwamba madaktari wanaendelea kumweka katika hali ya 'kuzirai kimatibabu', na kwamba yuko katika hali imara.
Bingwa huyo mara saba aligonga kichwa chake dhidi ya mwamba wakati akiteleza kwenye barafu katika milima ya Alps nchini Ufaransa.
Madaktari wanatumia madawa kumpa usingizi wakijaribu kupunguza uvimbe na kuchubuka kwenye ubongo wake.
Tayari wametekeleza upasuaji mara mbili kuondoa damu iliyoganda kwenye ubongo.
Hata hivyo huenda maisha yake yakawa hatarini iwamo ataendelea kuwa katika hali ya kuzirai kutokana na hatari ya ubongo wake kuharibika na kupata maambukizi ya kifua.

Friday, 27 December 2013

FALCAO: RONALDO NI MCHEZAJI BORA ZAIDI YA LIONEL MESSI

 
Mshambuliaji wa Monaco  Radamel Falcao anaamini kwamba mshambuliaji wa Real Madrid  Cristiano Ronaldo ni mchezaji mzuri kuliko staa wa klabu ya Barcelona Lionel Messi.

Mchezaji huyo wa Colombia anawakubali wachezaji wote wawili, ingawa Falcao anaamini Cristiano ni bora zaidi ya Messi.

"Messi na Cristiano ni wachezaji muhimu na wakubwa duniani leo hii lakini, kwangu mimi naamini Ronaldo ni bora zaidi," alisema mchezaji huyo mwenye miaka 27 alipoongea na El Tiempo.

Falcao pia amesema ni Cristiano Ronaldo anayestahili kuwa mchezaji bora wa dunia katika tuzo za Ballon D'or zitakazotolewa mwezi ujao ambapo Ronaldo anapambana na Ribery pamoja na Messi.

MCHEZAJI WA BORA WA LIGI YA BRAZIL - EVERTON RIBEIRO ASEMA ATAICHAGUA MAN UNITED MBELE YA REAL MADRID

 
Kiungo wa kibrazil Everton Ribeiro kwa mara nyingine ameelezea matamanio ya kujiunga na klabu ya Manchester United. 

United iliwatuma maskauti wake wa vipaji kwenda nchini Brazil kumuangalia staa huyo wa timu ya Cruzeiro na kocha David Moyes anafikiria kutuma ofa rasmi ya £12million ili kukamilisha usajili wa kiungo huyo, ambaye mwezi uliopita alishinda tuzo ya kuwa mwanasoka bora wa ligi ya Brazil.

Hata hiyo, United watakabiliana na upinzani kutka kwa Liverpool na Real Madrid ambao nao wamevutiwa na mchezaji huyo.

Ribeiro ambaye huko nyuma aliwahi kucheza katika mashindano ya vijana na United alipoulizwa na Globoesporte kama angependelea kujiunga na United badala ya Madrid, kiungo huyo mwenye miaka 24 alisema: ‘Ndio, ningependea kucheza United, mfumo ambao United wanaendesha timu ni bora kabisa duniani. Nimewahi kuwepo mahala pale na pia nilienda kupata mafunzo kutoka Alex Ferguson nilipokuwa kinda. ’

Wakala wa mchezaji huyo Robson Ferreira hivi karibuni alinukuliwa akisema: Manchester United wanamtaka Ribeiro,  David Moyes amevutiwa sana. Nilishaenda England na nikaongea rasmi na United.’

Tuesday, 24 December 2013

Juma Kaseja atetea bao alilofungwa


KIPA mwenye heshima kubwa nchini ambaye sasa anaichezea Yanga, Juma Kaseja amewaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba hakufungwa makusudi bao la tatu dhidi ya Simba kwenye mechi ya Mtani Jembe. Simba ilishinda mabao 3-1.
Kaseja alifungwa bao hilo dakika ya 62 baada ya kushindwa kumiliki vizuri mpira aliorudishiwa na Mbuyu Twite, ambapo mshambuliaji wa Simba, Awadh Juma alimuwahi na kumpokonya mpira halafu akafunga.
“Lengo lilikuwa nimiliki mpira na kupiga sehemu nyingine, sasa wakati nafanya hayo ndipo nilipowahiwa na jamaa akafunga. Hakuna maana nyingine hapo hilo ni kosa la kimchezo.”
Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Minziro alisema; “Kipa yeyote anaweza kukutana na hali kama ile, haifai kumlaumu Kaseja moja kwa moja tunapaswa kutazama tatizo la timu na kurekebisha makosa yetu.”
Licha ya kufungwa bao hilo lililozua mjadala kwa mashabiki wa Yanga, Kaseja alifanya vizuri kipindi cha kwanza kwa kuokoa hatari nyingi zilizokuwa zikielekezwa langoni kwake.
Kaseja anaichezea Yanga kwa mara ya pili baada ya kuwahi kufanya hivyo mwaka 2008 akitokea Simba kabla ya kurejea tena katika klabu hiyo hiyo mwaka 2011.

Wanaotesa kwa kutumia miguu ya kushoto Ligi Kuu England

LIGI Kuu England kwa miaka mingi tu imeshuhudia vipaji vya uhakika vya wachezaji wanaotumia miguu ya kushoto. Baada ya Mjerumani Mesut Ozil kutua Arsenal, huku Gareth Bale akihamia Hispania, bado kwenye ligi hiyo kuna wachezaji wanaotisha kwa ufundi wa kutumia miguu ya kushoto.
5. Moussa Dembele - Tottenham
Mbelgiji mwenye uwezo mkubwa wa kutamba kwenye safu ya kiungo na msumbufu wa wapinzani. Kwenye kulifanya hilo, silaha kubwa ya staa huyo ni mguu wake wa kushoto unaomwezesha pia kupiga mashuti makali. Uwezo wake wa kuwachambua wengine kwenye sehemu ya kiungo umemfanya afananishwe na Patrick Vieira. Ujuzi wake wa kumiliki mpira umewafanya wachambuzi wa soka kumfananisha na Ozil, lakini kazi kubwa inafanywa na mguu wake wa kushoto.
4. John Arne Riise - Fulham
 
Ujuzi wake alianza kuonekana wakati alipokuwa kwenye kikosi cha Liverpool kabla ya kuhamia Fulham. Amekuwa akifunga mabao muhimu kwenye kikosi hicho. Uwezo wake wa mguu wa kushoto umemfanya aimudu vyema nafasi ya beki wa kushoto na winga. Staa huyo wa Norway pia ni fundi wa mipira iliyokufa.
3. Robin van Persie - Man United
 
Kwenye orodha ya washambuliaji wa Ligi Kuu England kama kuna mchezaji ambaye mabeki wanakuwa na hofu pindi mpira unapokuwa kwenye mguu wake wa kushoto basi ni straika wa Kidachi, Robin van Persie.
Fowadi huyo anafahamu namna ya kuutumia mguu wake huo na kufunga mabao ya aina tofauti ikiwamo mipira ya adhabu. Hakika ndiye straika anayetisha zaidi na mguu wake wa kushoto.
Moja ya mabao yake ni lile alilofunga akiwa Arsenal kipindi ilipomenyana na Charlton Athletic, bao ambalo linatajwa kuwa bora zaidi lililowahi kufungwa kwa mguu wa kushoto kwenye Ligi Kuu England.
2. Mesut Ozil - Arsenal
 
Ndiyo yuko katika msimu wa kwanza kwenye Ligi Kuu England, lakini tayari ameonyesha cheche kali kutokana na ujuzi mkubwa wa kucheza soka kwa kutumia mguu wake wa kushoto.
Mguu huo ndiyo uliotengeneza nafasi kadhaa za kufunga kwenye ligi hiyo na kuipa faida kubwa Arsenal msimu huu kwenye Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akiwa amewahi kuwa chini ya Jose Mourinho walipokuwa pamoja Real Madrid, Mreno huyo alikiri kwamba hakuna mchezaji mwenye ujuzi wa kutumia mguu wa kushoto kama alivyo Ozil.
1. Ryan Giggs - Man United
Gwiji lao. Giggs kwa karibu miongo miwili mfululizo amekuwa akiwakimbiza mabeki wa timu pinzani kwa kutumia mguu wake wa kushoto na kuwa mchezaji mwenye hadhi kubwa kwenye Ligi Kuu England. Umahiri wa mguu wake huo umemtambulisha kiungo huyo wa Manchester United kuwa nyota hatari kwa miaka yote 20 aliyodumu kwenye ligi hiyo.
Amefunga mabao zaidi ya 114 kwenye kikosi hicho cha Manchester United, huku bao lake alilofunga dhidi ya Arsenal kwenye Kombe la FA likibaki kuwa kwenye kumbukumbu ya kipekee.

Sunday, 22 December 2013

DIAMOND,PENNY WAMWAGANA!

CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS
NDIYO habari ya ‘mujini’ kwa sasa, kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, mtangazaji wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ wamemwagana, Risasi Jumamosi limemwagiwa upupu.
Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ wakiwa pamoja katika pozi.
KAMA UTANI, WEMA ATAJWA
Kwa sharti la kutotajwa mahali popote, ‘mtonyaji’ wetu ambaye ni mtu wa karibu wa wawili hao aliliambia gazeti hili kuwa chanzo cha Diamond na Penny kuingia kwenye listi ya ‘zilipendwa’ kilianza kama utani.
Awali ilidaiwa kuwa kila mmoja amekuwa akijiona mwenye thamani mbele ya mwenzake huku Wema Sepetu naye akidaiwa kuwa chanzo.
                                Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Wema Sepetu.
“Hakuna penzi tena kati yao, wameachana na kila mmoja yuko kivyake.
“Walianza kama utani, unajua wale kila mmoja anajiona yuko juu kuliko mwenzake, lakini kitendo cha Diamond kuripotiwa kutoka na wanawake tofauti mara kwa mara hasa Wema, kimemchosha Penny ndiyo maana ameamua kujiweka pembeni kuepuka msongamano.
“Kupangwa kama mafungu ya nyanya inahusu?” alihoji ‘kikulacho’ huyo ambaye ni rafiki wa Diamond.

RISASI MZIGONI
Baada ya kutojiridhisha moja kwa moja na taarifa za awali kutoka kwa rafiki huyo, timu ya gazeti hili kwa kuwatumia ‘wahangaikaji’ wake maalum, iliingia mzigoni kupeleleza ukweli juu ya tetesi hizo.
Watu kadhaa walio chini ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo rais wake ni Diamond walihojiwa ambapo majibu yalikuwa yaleyale kwamba, kwa sasa Diamond na Penny imebaki stori!

 SHAKA ILIPOANZIA
Wakati timu yetu ikiendelea na uchunguzi wake makini juu ya uvumi huo, hivi karibuni Diamond alionekana ‘singo’ kwenye pati ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya ‘dada wa mjini’, Halima Haroun ‘ Halima Kimwana’ ambayo aliiandaa Diamond.
Minong’ono ya kuhoji kutoonekana kwa Penny ilisikika ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar ilikofanyikia pati hiyo iliyojaa vitendo vya ufuska.
“Haiwezekani leo rais (Diamond) akajiachia peke yake bila Penny. Si kawaida ya Diamond.
“Kwa vyovyote watakuwa wameshamwagana kwa sababu kwenye pati zote huwa wanakuwa pamoja tangu walipoanza uhusiano wa kimapenzi,” alisikika mmoja wa waalikwa katika sherehe hiyo.
Katika tukio hilo, Penny alipigiwa simu na paparazi wetu na kujibu kwa kifupi: “Naumwa. Halafu si lazima nije kwani kila mtu ana ratiba zake.”
                                                                Penniel Mungilwa ‘Penny’.
PENNY KIZIMBANI TENA
Baada ya kukamilisha udadisi huo kupitia kwa watu wao wa karibu, gazeti hili lilianza na Penny kwa kumuuliza undani juu ya habari hiyo lakini alionekana kuwa ‘mzito’ kwa kutoingia ndani kulizungumzia sakata hilo huku akiahidi kulifungukia muda wowote kuanzia sasa.
“Kwa sasa sina cha kuzungumza juu ya hilo, nitalizungumzia muda wowote tena si siku nyingi zijazo, lakini si leo, tafadhali sana,” alijibu Penny kwa kifupi na sauti ya chini iliyojaa uchovu.
Paparazi: “Hebu nisaidie, mko wote au hamko wote?”
Penny: “Nimesema sitoweza kusema lolote kwa leo, subirini.”
                                               Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’.
DIAMOND KIMYA
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu yake ya kiganjani, hakupokea licha ya kupigiwa mara kadhaa kwa namba zake zote. Akatumiwa meseji yenye maelezo yote, hakujibu.

MAMA DIAMOND
Ili kujiridhisha na madai hayo, waandishi wetu walimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye alisema hajui na hana taarifa hizo.

NDUGU WA KARIBU SANA
Baada ya mama Diamond, paparazi wetu alimpigia simu ndugu wa karibu sana na Diamond, sikiliza:
Paparazi: “Kumbe Diamond na Penny wamemwagana we huniambii. Sasa wifi yako mpya ni nani?”
Ndugu: “Aka! Sikwambii. Kwanza mi nipo mbali, sipo Dar.

WADAU WANAJUA
Haikuishia hapo, timu yetu ilizungumza na wadau mbalimbali ambao walionesha kusikitika huku baadhi yao wakisema walitabiri tangu awali.
“Duh! Penny ameachia ngazi mwenyewe. Sisi tulijua hawawezi kufika mbali, maana penzi lenyewe lilikuwa na mbwembwe nyingi,” alisema mwanamke mmoja anayejua kila kitu.

TUJIKUMBUSHE
Siku za hivi karibuni Diamond alifanya mahojiano kwa njia ya mtandao mmoja wa kijamii ambapo moja kati ya maswali aliyoulizwa ni pamoja na mpango wa kuoa ambapo alisema kuwa hana mpango huo kwa sasa na hatarajii kumuoa yeyote kati ya wanawake wanaotajwa kwa sana midomoni mwa watu (akiwemo Penny).
Wema alipigiwa simu juzi, lakini simu yake ilikuwa ikiita ‘weee’ mpaka inakatika, inaita ‘weee’ mpaka inakatika.

MATOKEO EPL JANA: LIVERPOOL WASHIKA USUKANI


Wachezaji wa Liverpool wakimpongeza Luis Suarez (wa pili kulia) baada ya kuwafungia moja ya bao dhidi ya Cardiff leo
Jesus Navas akishangilia bao la tatu aliloifungia Manchester City dhidi ya Fulham leo.
Danny Welbeck akishangilia bao la kwanza kwa Manchester United dhidi ya West Ham jana
Manchester United 3-1 West Ham, Liverpool 3-1 Cardiff, Fulham 2-4 Manchester City, Crystal Palace 0-3 Newcastle, Stoke 2-1 Aston Villa, Sunderland 0-0 Norwich, West Brom 1-1 Hull. Kwa matokeo ya jana, Liverpool wameongoza Ligi Kuu ya England wakiwa na pointi 36 wakifuatiwa na Manchester City pointi 35 na Arsenal pointi 35!

Friday, 20 December 2013

Klabu bingwa ya dunia ni Raja au Bayern?

Timu ya Raja Casablanca kutoka Morocco imefuzu kucheza fainali za klabu bingwa ya dunia baada ya kuisambaratisha Atletico Mineiro kutoka Brazil katika mchezo wa nusu fainali.
Raja waliweza kufunga magoli mawili katika dakika 10 za mwisho katika mchezo huo.
Kwa matokeo hayo Raja Casablanca watamenyana na Bayern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa fainali.
Raja ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia bao lililofungwa na Mouhssine Lajour.
Mchezaji wa zamani wa Barcelona Ronaldinho alipiga kiufundi mpira wa adhabu na kuisawazishia bao timu yake ya Mineiro.
Lakini Mohaine Moutaouali aliiweka mbele timu yake ya Raja baada ya kufunga mpira wa penalti, huku Vivien Mabide akikamilisha ushindi wa magoli 3 ya Raja dhidi ya 1 la Mineiro.
Kivutio katika mchezo ni kwa wachezaji wa Raja kumzunguka Ronaldinho mara baada ya kupigwa filimbi ya kumaliza mchezo, huku wakimbusu na jezi na viatu vyake kama kumbukumbu tosha ya kucheza dhidi ya nyota huyo wa Brazil.
Ronaldinho mwenye umri wa miaka 33 amewahi pia kuvichezea vilabu vya St-Germain ya Ufaransa, AC Milan ya Italia pamoja na Barcelona ya Hispania, huku pia akiichezea timu yake ya taifa ya Brazil.
Mchezaji huyo bora wa zamani wa mwaka, ameichezea timu yake ya taifa mara 90 na ana matumaini kuwa atakuwa miongoni mwa kikosi cha Brazil kitakachocheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014, zinazoandaliwa nchini Brazil mwakani.
Kouko Guehi na Vivien Mabide wa Raja Casablanca walishangilia wakiwa na viatu vya Ronaldinho baada ya kushinda mchezo huo wa nusu fainali za kombe la klabu bingwa ya dunia dhidi ya Atletico Mineiro.
Raja sasa itapambana na mabingwa wa Ulaya Bayern Munich katika fainali itakayochezwa Jumamosi huko Marrakesh.
Hii ni mara ya pili kwa fainali hizo kutozikutanisha timu za Amerika Kusini na Ulaya katika mchezo wa fainali, tangu michuano hiyo kuchezwa katika muundo wa sasa ulioanza mwaka 2005.

Thursday, 19 December 2013

Ismail Aden Rage kakubali kujiuzulu,ila hiki ndicho alichokisema


ragee                                                Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage
Wanachama wa klabu ya Simba wamemjia juu Mwenyekiti wake Ismail Aden Rage juu ya suala zima la mchezaji Emanuel Okwi,Hivi ndivyo alivyosema Rage ‘Mimi najiuliza ndo maana nimeomba ufafanuzi toka Fifa baada ya kufika tu,mi nilikua sipo nchini kwa mwezi mzima nimeandika barua kwenda Fifa jana ile ile na pia Tff tumeandika barua kwa niaba ya Simba ili kutoa malalamiko yetu,kwa sababu hata sisi inatuchanganya huyu mchezaji mkataba wake,labda kama kuna ushahidi watuonyeshe kama Fifa wamevunja mkataba na Etoile du Sahel  lakini ukisoma kwenye mtandao wa Fifa kuna kesi 3 ziko pending’.
‘kesi ya Simba kuidai Etoile du Sahel  kuna kesi ya Etoile du Sahel  kulalamika mchezaji wao ametoroka,kuna kesi ya Emanuel Okwi kudai pesa zake hajalipwa na Etoile du Sahel,kwa hiyo huu ujanja uliotumika sijui umetokea wapi tumelalamika Fifa wakati tunamtoa Villa walisema wamempeleka Villa kwa mtaba wa miezi 6 na miezi 6 haijaisha,jana nimeona kwenye luninga  moja wanaonyesha ITC ile ITC kila club Tanzania inawezaa kuprint tu.’
‘Uganda matatizo yao walisaidiwa kutatuliwa kwa haraka na chama chao cha mpira cha Uganda sisi chama chetu hapa lazima niseme ukweli hawajatusaidia vya kutosha wamelala kwa muda mrefu sijui  kwa sasa hivi kwa sababu amekuja  mheshimiwa Malinzi labda wataanza kusaidia vilabu vytu kuhakikisha tunapata haki zetu kwa sababu Fifa wana utaratibu wao wa kuheshimu wanachama wao wanatoa uzito kwa mfano Sector General wa Fifa anaweza kuongea na Sector General wa tff lakini si mimi President wa Simba,siwez kuongea na Sector General wa Fifa moja kwa moja  mi naongea na makanjanja tu’.
‘Kwenye sheria tuna kitu kinaitwa Legal Status Kwa wanachama wa tawi la Mpira Pesa hawana hadhi ya kisheria ya kuongea masuala ya simba maana hao si tawi la simba lililosajiliwa hawana hata hiyo hati na haiwezekani katika matawi 78 tawi 1 tu kila siku wanaongea mi wangeongea matawi 78 kidogo ningeshtuka ,mimi nimechaguliwa na watu 1,820 sasa tawi la mpira pesa sijui lina watu 204 sijui 100 ila hata sielewi lina watu wangapi,haliwezi kunipa taabu’.
‘Sina nia ya kuitisha mkutano wa dharura kama hali itaendelea hivi ya kutoelewana njia nyepesi nayoona ndugu yangu ni kuitisha mkutano wa uchaguzi mwezi January kabla ya tarehhe 27 Januaryili upatikane uongozi mpya  kuanzia Mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji’
‘Napitia vifungu vya sheria nisome na ngojea uamuzi wa Tff watasema nn kuhusu malalamiko yangu,maana baada ya maazimio ya kamati utendaji  niliandika barua kuomba kamati ya utendaji ipitie maamuzi yake ya mwanzo kulikua na dosari nilizona na nikaeleza dosari nilizoziona kwa hiyo wakirekebisha hizo dosari nipo tayari kufata’
‘Mimi binafsi siwezi kufanya kazi na kamati ambayo tayari  ilishanituhumu  na kunisimamisha kwa hiyo tayari hawana imani na mimi sasa mimi imani na wao natoa wapi,kwa hiyo tutakua hatuwatendei haki wanachama wa Simba,sasa ili tuonekane wote tunafata maadili basi ni vyema kuanzia Mwenyekiti na Wajumbe wote wa kamati ya utendaji tukajiuzulu tukaitisha mkutano wa uchaguzi  ili kuikoa klabu yetu ili ipate mafanikio makubwa’.

SAMUEL ETO'O ASHAMBULIWA NA MASHABIKI WA CHELSEA


240913etoo-samuelMashabiki wa Chelsea wanamrushia matusi pamoja na maneno ya kebehi striker Samuel Eto’0 baada ya kupost picha ambayo sio kawaida kwa mchezaji ku-tweet pale timu yake inapokua imepata matokeo mabaya uwanjani.
Picha yenyewe ni hii hapa chini inaonyesha matokeo ya Chelsea dhidi ya Sunderland then Samuel Eto’o aka-tweet kwa followers wake zaidi ya laki moja na nusu kitu ambacho baadhi yao wamekichukulia vibaya kwamba kwa nini timu ifungwe alafu apost?
etoo
Hizi ni baadhi ya tweets kutoka kwa mashabiki ambapo tweet nyingine zina maneno mazito kutoka kwa mashabiki hawa ambao wamemjibu Samuel.e1
e2
e3
e4

Monday, 16 December 2013

DUNIANI WAWILI WAWILI.MCHEKI JAMAA ANAFANANA NA NGWEA COPYRIGHT


ngwea2
Tamasha la Xxl Afta xkul Bash ndio sehemu ambayo nilimuona huyu jamaa baada ya kujitokeza kwenye mashindano ya kumtafuta Mtu anaefanana na Star.
Nikaona si mbaya tukafahamu hata kwa uchache historia yake na anamjua vipi Marehemu Ngwea.
ngwea‘Mi naitwa Mohamed au Junior weezy, junior weezy kwa sababu imekua Talk of Town gumzo Town kila mtu Ngwea Ngwea,mi Ngwea namfaham kama artist so nimeonana nae mara ya mwisho nikiwa mdogo lakini Jay Moe alimwambia Ngwea unafanana sana na jamaa pale ndo ilikua mara yangu ya kwanza naya mwisho kuonana na Ngwea’.
ngweaaa‘Yeah ilikua mwaka 2003 baada ya Jay Moe kumwambia unafanana sana na dogo alisema ndio kweli nafanana nae lakini mtu aliekuja kunifahamisha zaidi ni Dully,Dully alisema unafanana sana na Ngwea na mpaka leo huwa ananiita Ngwea.watu walinishawishi kulingana na hii sura nliyonayo watu wamenishawishi taratibu naanza kuingia kwenye game bado sijafanya track nipo njiani,nakutana na vituko vingi wengine wananikimbia wanasema nimefufuka na vitu vingine vya ajabu nakutana navyo mtaani muda mwingine nasisimka nahisi kama Mangwea yuko ndani ya mwili wangu,naweza kuimba baadhi ya ngoma za Ngwea kama tupo juu..na baadhi ya ngoma zingne.
ngweeeeaaa
ngwea na mox
ngweaaa

EXCLUSIVE!!!!!RATIBA YA LIGI YA MABINGWA ULAYA HII HAPA......

Celtic supporters at the Champions League encounter against AC Milan
Tue 18 Feb 2014 - Champions League
  • Bayer 04 Leverkusen   v        Paris Saint Germain 19:45
  • Man City                       v       Barcelona 19:45
Wed 19 Feb 2014 - Champions League
  • Arsenal                         v         Bayern Munich 19:45
  • Milan                            v         Atlético Madrid 19:45
Tue 25 Feb 2014 - Champions League
  • Zenit St Petersburg      v         Borussia Dortmund 17:00
  • Olympiakos                  v         Man Utd 19:45
Wed 26 Feb 2014 - Champions League
  • FC Schalke 04             v         Real Madrid 19:45
  • Galatasaray                 v         Chelsea 19:45

Saturday, 14 December 2013

MECHI ZA KESHO 15/12/2013 LIGI KUU UINGEREZA

15 Dec 2013 - Premier League
  • Aston Villa       v        Man Utd 
  • Norwich           v        Swansea 
  • Tottenham        v       Liverpool

MATOKEO YA LIGI KUU ENGLAND LEO 14/12/2013

  • Man City       6 - 3     Arsenal FT
  • Cardiff           1 - 0     West Brom FT
  • Chelsea          2 - 1     Crystal Palace FT
  • Everton          4 - 1     Fulham FT
  • Newcastle      1 - 1     Southampton FT
  • West Ham      0 - 0     Sunderland FT
  • Hull                0 - 0     Stoke

Kenya yakata keki miaka hamsini!

Kenya inafikisha miaka hamsini Alhamisi hii tangu kujitatawala miaka hamsini iliyopita.
Kumbukumbu , maoni, mageuzi, yote haya na mengi mangineo yanajitokeza katika umuhimu wa kusherehekea mwaka huu wa Jubilee.

Mnamo mwaka 1998, watu 224 walifariki wakati kundi la kigaidi la Alqaeeda liliposhambulia ubalozi wa Marekani nchini Kenya .
Wakati huu ambapo Kenya inafikisha umri wa makamo, ni jambo la kawaida kwa watu kusahau baadhi ya vitu. Unaweza kupoteza funguo zako, hata usahau filamu uliyoitizama mwezi jana, Kenya pia inaonekana kusahau haraka.
Kabla ya mashambulizi ya kigaidi kufanyika dhidi ya jengo la Westgate mjini Nairobi mwezi Septemba ambako mamia walijeruhiwa na wengine kuuawa, Kenya iliwahi kukabiliana na hali kama hii, mashambulizi mabaya zaidi hata kuliko ya Westgate ambayo yalilenga ubalozi wa Marekani mjini Nairobi.
Lakini mafunzo ambayo Kenya ingetoa kwa mashambulizi ya kigaidi yakawa yamesahahulika.

Maono

80% ya wakenya wako chini ya umri wa miaka 35.
Mabadiliko katika umri yanapaswa kuleta mabadiliko katika maono.
Tunapoendelea kuzeeka, Kenya inahitaji miwani kuona vyema zaidi.
Kisheria Kenya inaonekana kuzeeka kabisa.
Na nchi inapoendelea kuzeeka imekosa kuona kuwa idadi ya vijana inaongezeka maradufu
Asilimia themanini na wakenya wako chini ya umri wa miaka 35, na kila mtoto anapozaliwa, anahitaji kupangiwa elimu, kulishwa, huduma ya afya na ajira. Lakini licha ya idadi ya watu kuongezeka, ni vijana ambao wanakabiliwa na changamoto ya ajira.
Idadi ya watu Kenya imeongezeka zaidi ya mara nne tangu nchi hiyo kujipatia uhuru.
Asilimia 42% wako chini ya umri wa miaka 15. Idadi ya watoto wanaofariki wakizaliwa imepungua. Vijana hawana ajira na hao ndio wengi zaidi. Kenya inahitaji kuona vyema inachohitaji kufanya kubadili hali wakati inaposherehekea miaka hii hamsini ya Uhuru wake.

Harakati

Kumekuwa na maandamano ya kila aina kuonyesha ghadhabu juu ya wabunge kujiongeza mishahara mwaka huu.
Serikali haikusikia kilio hicho na wabunge waliweza kupata walichokuwa wanataka.
Kabla ya uchaguzi mwezi Machi, wananchi waliandamana kwa hasira wakiwalaani wabunge waliokuwa wanawaibia pesa zao ili kujipa maisha mema, lakini kwa hofu ya kutopigiwa kura , waliamua kutojiongeza mishahara hiyo wakati huo hadi pale uchaguzi ulipokamilika.
Serikali haikusikia kilio cha wananchi , wabunge sasa wako sawa maana walikipata walichokitaka.
Yote tisa, kumi ni kuwa Kenya inaposherehekea miaka hamsini ya uhuru wake, kuna mengi ambayo serikali inaendelea kupuuza . Na kwa mwananchi wa kawaida itachukua muda labda miaka mingine hamsini kwake kuona mafanikio ya juhudi za wakombozi na wazalendo waliopigania uhuru.
- See more at: http://www.helperblogger.com/2012/06/jquery-facebook-like-box-popup-with.html#sthash.AGJhd6Gy.dpuf