WANAFUNZI 12 wa Shule ya Sekondari ya Mlowa iliyopo Wilaya ya Iringa Vijijini wamenusurika kufa baada ya bweni walilokuwa wamelala kuungua kwa moto na kuteketeza vitu ambayo vilikuwemo ndani.
Tukio hilo linadaiwa lilitokea
baada ya hitilafu ya umeme wa nishati ya jua (Sola) iliyosababishwa na
wanafunzi ambao walikuwa wamelala katika bweni hilo kuunganisha nyaya kienyeji kwa ajili ya
kusikiliza redio na kusababisha hasara ambayo inakadiriwa kufikia sh. milioni
1.8.
Akizungumzia jana ofisini kwake juu ya tukio hilo la kuungua kwa
bweni na kunusurika kwa wanafunzi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mlowa, Mwalimu
Frank Mahai alisema wanafunzi wa l i o n u s u r i k a awa l i walikuwa
wanaishi nje ya shule.
Alisema, mipango ya kuishi katika bweni hilo ilifanywa katika kikao cha wazazi na walimu kwa ajili ya wanafunzi ambao wanatoka mbali na shule ili wapate mahali pa kuishi katika muhula wa mitihani ya mwisho.
Mkuu huyo alisema kuwa, wanafunzi wengine wa shule hiyo wakati
inaungua walikuwa wamekwenda kucheza mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana
katika Shule ya Sekondari ya Kalenga na kubakia wanafunzi 12 katika bweni
ambapo saa 1:30 jioni moto ulianza kuunguza bweni hilo.
“Wanafunzi waliohusika na kuunguza ni baada ya kuunganisha nyaya
kienyeji na kusababisha shoti hadi kuunguza bweni hilo,” alisema Mkuu huyo.
Alivitaja vitu vilivyoungua kuwa ni pamoja na nguo za wanafunzi,
mabegi, madaftari, magodoro pamoja na paneli za sola ambazo zimeteketea moja
kwa moja pamoja na dari ya chumba cha bweni ambapo jumla ya gharama zake
zinafikia kiasi hicho cha fedha.
Hata hivyo Diwani wa Kata ya Mlowa, Charles Nyagawa (CCM)
akizungumzia tukio hilo alisema kuwa
amesikitishwa na kuungua kwa bweni hilo
ambalo wazazi walishiriki kujenga na walitumia gharama kubwa.
Diwani huyo alisema, amesikitishwa na tabia za wanafunzi kuunguza
bweni hilo
kutokana na kujiingiza kwenye ufundi ambao hawaujui na wala hawana utaalamu
nao.
Al i s ema k uwa , p i a anawashukuru wazazi na wananchi ambao walifika katika kijiji hicho na kuuzima moto na kuwa i n g awa h awa k uwe z a kufanikiwa anawashukuru kwa ushirikiano ambao w a l i u o n e s h a k a t i k a kuhakikisha moto huo unazimika na kuokoa baadhi ya mabweni mengine yasiendelee kuungua moto na kuteketea mali zingine zikiwemo za wanafunzi ambao walikwenda kwenye michezo na vitabu vya shule.
No comments:
Post a Comment