Klabu ya Liverpool imekubali kwamba inaweza kuumuza mshambuliaji wa kiuruguay Luis Suarez endapo tu timu inayomtaka italipa kiasi cha paundi millioni 50 - ambayo ndio thamani ya mshambuliaji huyo kwa mujibu wa Liverpool wenyewe.
Juzi
usiku klabu ya Arsenal ilivunja bank na kuamua kutoa ofa ya £40million
kwa Liverpool kwa ajili ya kumsaini Luis Suarez lakini majogoo wa jiji
wakaipiga chini ofa hiyo na kusisitiza kwamba ikiwa Arsenal wanahitaji
saini ya Suarez basi inabidi walipe fedha ambayo ni thamani ya kweli ya
mshambuliaji ambayo inatajwa kuwa £50m - kwa mujibu wa kocha wa
Liverpool Brendan Rogers.
"Ikiwa Arsenal wanamtaka Suarez, then inabidi walipe fedha ambayo inaendana na thamani ya kweli ya mchezaji."
Lakini huku Rogers akisema hivyo imeripotiwa kwamba Arsenal wanataka mshambuliaji mwenyewe alazimishe kuondoka na kujiunga nao.
Arsenal wanaamini kwamba Suarez ameshaamua kwa dhati kuondoka Anfield ili ajiunge na timu inayocheza soka la ligi ya mabingwa wa ulaya.
Na wanaamini ofa yao ya £40m imefikia fedha ambayo inatakiwa kuvunja mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 - kitu ambacho kinawapa ruhusa ya kuongea na mchezaji huyo.
Lakini tatizo kubwa kwa Arsenal ni kwamba wanaamini mshambuliaji huyo angependelea zaidi kujiunga na Real Madrid ambayo nayo imeomnyesha nia ya kumhitaji.

Real
Madrid jana walimuuza mshambuliaji wao Gonzalo Higuain kwenda Napoli
kwa ada ya uhamisho wa £32 +nyongeza, na hivyo wanaweza kuja kumalizana
na Liverpool muda wowote ikiwa wataachana na mpango wa kumsajili Gareth
Bale ambaye anaweza kuwagharimu kiasi kisichopungua £70m.
No comments:
Post a Comment