Blogger Widgets

Tuesday, 23 July 2013

SAKATA LA USAJILI WA CESC FABREGAS: ARSENAL HAWATOPATA CHOCHOTE KWENYE ADA YA UHAMISHO? ISIPOKUWA TU PALE ITAPOPATIKANA FAIDA YA MAUZO YA MCHEZAJI HUYO.

Ripoti kwamba Arsenal wana haki ya kupata 50% ya fedha za ada ya uhamisho ikiwa Cesc Fabregas atahama kutoka Barcelona kwenda Manchester United sio za kweli kabisa, kwa mujibu wa ESPN.
Leo, David Moyes amethibitisha United imetuma ofa ya pili ambayo inadhaniwa kuwa ni £30 million kwa ajili ya kumsaini mchezaji huo wa zamani wa Arsenal, na sasa wanasubiri majibu kutoka kwa mabingwa hao wa Spain. 

Huku sasa tayari kukiwa na ofa rasmi mezani, Barcelona wanapaswa kuwataarifu Arsenal na kuwapa nafasi ya kumsajili tena mchezaji huyo kwa bei watakayokubaliana.

The Gunners wana haki ya kumsaini tena Fabregas kwa ada ambayo ipo karibu na waliyotoa United.
Ikiwa watashindwa kufanya hivyo, watapokea 50% ya faida yoyote ambayo FC Barcelona watapokea ikiwa watamuuza Fabregas kwa klabu nyingine. Na kwa ada ya uhamisho wa £30million ni vigumu kwa Arsenal kupata chochote kwa sababu Barca watakuwa hawajatengeneza faida. 

Mpaka sasa boss wa Arsenal Arsene Wenger ameshaonyesha ishara kwamba hana mpango wa kumrudisha Fabregas jkaskazini mwa London, United wanaamini wanaweza wakafanikiwa kumsajili kiungo huyo wa Spain. 

Mapema mwezi uliopita, balozi wa klabu hiyo ya Old Trafford Denis Irwin alisema United "watafanya kila wawezalo kumsajili  Fabregas - lakini kuna vikwazo kadhaa vilivyobaki ili uhamisho huo ufanikiwe.
Haijawa wazi kwamba Fabregas angependelea kwenda kucheza Manchester miaka miwili baada ya kurudi kwenye klabu yake ya utotoni Barcelona.
Uwepo wa mchezaji mwenzie wa Arsenal wa zamani Robin van Persie ndani ya Old Trafford unaweza ukamhasisha Cesc kuhamia jijini Manchester, wakati uwezekano wa kucheza kila wiki ukiwa mdogo pale Nou Camp katika msimu wa kuelekea kwenye Worl Cup unaweza ukawa kishawishi kingine cha Fabregas kuamua kuhamia Manchester United.  

MUDA UTAONGEA ZAIDI

No comments:

- See more at: http://www.helperblogger.com/2012/06/jquery-facebook-like-box-popup-with.html#sthash.AGJhd6Gy.dpuf