Mume na mke wakiongea
Seleman Yasin (78), mkazi wa Mtaa wa Mtamba, Msasani jijini Dar es Salaam, juzi Alhamisi alizimia baada ya kupata taarifa za mkewe, Saida Abdalah ‘Mama Hamisi’ (21), kunaswa kwa tuhuma za ukahaba na kupandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Jiji.
Imedaiwa mahakamani hapo kuwa Mama Hamisi alinaswa kwenye msako wa machangudoa uliofanyika usiku wa kuamkia juzi maeneo ya Buguruni.
Akiwa kizimbani, Mama Hamisi alisomewa shitaka la kujiuza na mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi mbele ya Hakimu Timoth Lyon.
Baada ya kusomewa shitaka lake, Mama Hamisi na makahaba wengine 13, walikana kufanya biashara hiyo kesi ikaahirishwa hadi Julai 31, mwaka huu.
Hakimu Lyon aliwaambia washitakiwa kuwa dhamana iko wazi ndipo akatokea mume wa Saida ‘Baba Hamisi’ na kujitambulisha kisha kuanza kuhangaikia dhamana ya mkewe ambaye wakati huo tayari alikuwa nyuma ya nondo.
“Yaani we Mama Hamisi kila siku unanidanganya unauza ubwabwa, Buguruni kumbe ubwabwa wenyewe ndio huo! Akafyatua tusi,” Baba Hamisi.
“Kila siku mimi nalala nyumbani na watoto wewe unarudi alfajiri unanidanganya unauza ubwabwa!
“Mimi machale yalishawahi kunicheza kipindi fulani sema nilikuwa nakuvizia lakini leo Mungu kanionesha ,” alisema Baba Hamisi.
Licha ya kupandwa na jazba lakini mtu chake, Baba Hamisi alituliza jazba na kutaka kumchomoa kipenzi chake kwa dhamana lakini alishindwa kutimiza masharti.
Kwa kuwa Baba Hamisi alikuwa na safari ya muhimu ya mkoani ikabidi aondoke na kumuachia nguo za sikukuu alizonunua kwa ajili ya mtoto wao, Hamisi.
Akizungumza na mwandishi wetu, Baba Hamisi alisema yeye hakuwa akifahamu kama mkewe anajiuza hivyo tukio hilo lilisababisha apigwe na butwaa.
No comments:
Post a Comment