JOSE
MOURINHO amesisitiza kwamba sasa ni uamuzi wa mwisho kuhusu usajili wa
Wayne Rooney umebaki mikononi mwa klabu ya Manchester United.
Chelsea leo mchana ilithibitisha kwamba wametuma ofa rasmi ya kumsajili Rooney lakini United wameikataa
Lakini muda mfupi uliopita Mourinho amethibitisha kwamba Rooney ndio mchezaji pekee anayemhitaji kwenye kikosi chake.
"Nadhani kila kitu kipo wazi sasa - sio siri tena. Ofa rasmi imetumwa lakini ilikuwa ya kiasi cha fedha na haikuhusisha mchezaji yoyote. Tunamhitaji mchezaji. Tumetuma ofa na sasa hatuna cha kusema zaidi. Tumewaachia Manchester United waamue.”
NANI ZAIDI KITAKWIMU: WAYNE ROONEY VS JUAN MATA
Siku ya leo zilitoka taarifa kwamba Chelsea walituma ofa ya Paundi Millioni 10 pamoja na mchezaji mmoja aidha David Luiz au Juan Mata, ingawa muda mchache uliopita Chelsea walikanusha suala hilo - wakisema walituma ofa tu ya fedha.
Pamoja na hayo tu kumekuwepo na mjadala kama ni sahihi kwa United kukataa ofa ya 10m + Mata? Kama ni kweli Chelsea walituma ofa hiyo.
Lakini ebu tujaribu kutazama kitakwimu kwa msimu uliopita ni nani zaidi baina ya wachezaji hawa wawili.
CHELSEA YATHIBITISHA KUTUMA OFA YA KUMSAJILI WAYNE ROONEY - LAKINI YAKANUSHA KUTAKA KUWATOA AIDHA MATA AU LUIZ KWENYE DILI HILO
Lakini pamoja na kuthibitisha kutuma ofa hiyo, Chelsea wamekanusha taarifa kwamba ofa hiyo ilikuwa ni ya kiasi cha fedha pamoja kutoa mchezaji wao mmoja ili kuweza kumsaini Rooney.
Katika taarifa iliyotolewa na mtandao rasmi wa Chelsea - klabu imekiri kwamba jana usiku ilituma ofa kwenda United lakini haikuwa inahusisha mchezaji wao yoyote kuhusishwa na dili hilo.
TAARIFA RASMI YA CHELSEA KUHUSU OFA YA ROONEY
No comments:
Post a Comment