Blogger Widgets

Tuesday, 30 July 2013

KUTANA NA KINDA LA BURKINA FASO LILOMKUNA MOURINHO KWENYE PRE SEASON YA CHELSEA - AKIWA BADO SIO MCHEZAJI WA CHELSEA

Kinda la Burkina Faso Bertrand Traore ni mmoja wa makinda waliomvutia sana kocha wa Chelsea Jose Mourinho katika mechi za maandalizi ya msimu mpya huko barani Asia. 

Kwa sababu ya kanuni za usajili mchezaji huyo sio mchezaji rasmi wa The Blues mpaka atakapotimiza miaka 18 mnamo tarehe 6 September, hapo ndipo anaweza kusaini mkataba wa kuitumikia Chelsea.
Wiki hii katika mechi ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya  Malaysia XI alifunga bao zuri sana na akaongeza bao jingine katika ushindi wa 8-1 dhidi ya Indonesia All Stars.

"Ni kijana mdogo, lakini nina uhakika atakuja kuwa na umuhimu sana ndani ya kikosi cha Chelsea cha baadae," mchezaji mwenzie Gary Cahill alisema.

Traore alikuwa sehemu ya kikosi cha Burkina Faso kilichoshiriki michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika mwaka 2012 zilizofanyika Equatorial Guinea na Gabon - alicheza katika mechi aliyotokea benchi dhidi ya Sudan katika mchezo wa makundi.

Cahill anasema Traore sio muoga na anajiamini sana akiwa mazoezini akicheza na wachezaji wakubwa wa kikosi cha kwanza. 

"Ameweza kuingia vizuri kwenye timu ya wakubwa. Amezoea. Ni mapema sana kusema yupo tayari kucheza kwenye level ya juu, itakuwa sio vizuri akijiamini kupita kiasi." - Cahil

Traore hakuitwa na kocha Paul Put kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika mapema mwaka huu huko Afrika ya Kusini, ambapo timu yake ilienda na kushika nafasi ya pili nyuma ya Nigeria. Lakini amekuwemo katika kikosi cha sasa ambacho kipo katika nafasi nzuri ya kufuzu kuingia kwenye hatua ya mtoano ya michuano ya kufuzu kombe la dunia. 


Mapema January 2011, Traore alikaririwa akiongea na kipindi cha Fast Track cha BBC akisema; "Nataka kucheza kwenye kikosi cha kwanza Chelsea, nataka kucheza kwenye Champions league na timu zenye majina makubwa.

"Nataka kucheza kila mechi ya timu ya Chelsea na huko mbeleni ningependa kuja kuwa mchezaji bora kutoka Afrika kuichezea Chelsea."

No comments:

- See more at: http://www.helperblogger.com/2012/06/jquery-facebook-like-box-popup-with.html#sthash.AGJhd6Gy.dpuf