Blogger Widgets

Sunday, 28 July 2013

KIUNGO WA AZAM HUMPHREY MIENO ATAJWA KWENDA KUZIBA NAFASI YA WANYAMA CELTIC


Victor Wanyama ameondoka Celtic Football Club na kujiunga na klabu inayoshiriki kwenye ligi kuu ya England - Southampto baada ya kukamilisha uhamisho wa wa £12.5million. Sasa ikiwa ni wiki kadhaa tangu kiungo huyo wa Kenya kuondoka, kocha wa Celtic Neil Lennon, amesema Wanyama alikuwa ndio kiungo wake bora wa ushambuliaji kwenye timu yake na sasa wanahitaji mbadala wake.
Kutokana na hilo sasa zimeibuka taarifa kwamba kocha huyo ambaye ni nahodha wa zamani wa Celtic anamuwania kiungo mwingine kutoka Kenya Humphrey Mieno. Mieno ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Azam FC  inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Tanzania.
Celtic, itabidi ifanye haraka kumsaini mchezaji huyo wa Azam FC kwa kuwa kuna vilabu vingi barani Afrika kama miamba ya soka ya Tunisia Esperance na Club Africain zinamuwania kwa nguvu mchezaji huyo ambaye alihamia Azam akitokea Sofapaka ya Kenya.
Mpaka sasa sio Celtic wala Azam FC ambazo zimethibitisha kuhusu taarifa hizi.

No comments:

- See more at: http://www.helperblogger.com/2012/06/jquery-facebook-like-box-popup-with.html#sthash.AGJhd6Gy.dpuf