Katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah amesema TFF hawana taarifa za alipokwenda Kazimoto zaidi ya kusikia kuwa amekwenda kusaka timu nchini Qatar,kitendo ambacho wanachukulia kama utovu wa nidhamu.
Angetile amesema Kazimoto amevunja kanuni za kambi ambazo anazifahamu na wachezaji wote wa Taifa Starz wanafahamu kanuni hizo ambazo wanapewa wanapoingia kwenye kambi ya timu ya Taifa.
Itakumbukwa kwenye msimu uliopita wa ligi kuu ya Tanzania bara Kazimoto alisimamishwa na timu yake ya Simba kwa utovu wa nidhamu kabla ya baadaye kurejeshwa kundini
No comments:
Post a Comment