Blogger Widgets

Tuesday, 26 November 2013

Abiria waingizwa mjini kituo kikuu cha mabasi ya mikoani ubungo

 
Wauziwa tiketi za basi ambalo halipo kabisa katika eneo la maegesho ya kituo hicho.
Dar es Salaam. Abiria waliokuwa wasafiri kwenda Korogwe kwa basi (jina tunalihifadhi) wamekumbana na utapeli wa aina yake baada ya kuelezwa kuwa basi hilo halipo. 
Blog hiii ilishuhudia baadhi ya abiria wakifika kwenye ofisi ya basi hilo kutaka kurudishiwa fedha zao huku wengine wakipigwa butwaa kituoni hapo baada ya kuambiwa basi halipo.
Hata hivyo, mmoja wa abiria alisema kuwa, walichukua hatua hiyo kutaka kurudishiwa fedha zao baada ya kuona hakuna dalili za basi hilo licha ya kutakiwa kuripoti saa 4:30 asubuhi.
Akizungumza  mwanadada ambaye hata hivyo alisema si msemaji, alidai kuwa gari lao limepata pancha hivyo haliwezi kusafiri.
BLog ilipohoji pancha hiyo ni ya kiasi gani mpaka wafute safari, mwanadada huyo alionekana kubabaika lakini alisisitiza kuwa basi hilo limeshindwa kusafiri kutokana na hali hiyo.
Mmoja wa abiria waliokuwa wasafiri na basi hilo alisema, utapeli kama huo umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu kituoni hapo kwa kuwakatia tiketi abiria na kuwaonyesha gari huku wakifahamu wazi kuwa gari husika halipo na kinachofanyika kesho yake ni kupewa gari tofauti na makubaliano ya awali.
Blog ilishuhudia abiria hao waliokuwa wasafiri na basi hilo wakifaulishwa kwenye basi lingine ambalo halifanani kabisa na lililochapishwa kwenye tiketi za basi walilotarajiwa kuondoka nalo.
Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida ikionekana kinachofanyika katika kituo hicho kinafahamika wahudumu wa basi hilo lililoondoka walizichukua tiketi za basi lililodaiwa kuwa ni bovu na kuwapa tiketi nyingine na kuendelea na safari. Matukio kama hayo yamekuwa yakishamiri kituoni hapo hasa mwishoni mwa mwaka.

No comments:

- See more at: http://www.helperblogger.com/2012/06/jquery-facebook-like-box-popup-with.html#sthash.AGJhd6Gy.dpuf