Wapelelezi
wa Uingereza wanafanya uchunguzi juu ya tukio la kukaribia kugongana
kwa ndege mbili aina ya Jumbo Jet hivi karibuni kwenye anga ya Scotland
ambapo ndege hizo aina ya Jumbo Jet 747 zilikaribia kugongana zikiwa
hewani saa chache baada ya kupaa huku zikiwa zimebeba abiria zaidi ya
elfu mojaWaongozaji wa ndege hizo wanasema kuwa marubani wa ndege hizo hawakufuata maelekezo sahihi ambapo rubani mmoja aliomba kupewa maelekezo na alielekezwa kwenda kuifuata ndege nyingine jambo ambalo lingesababisha ajali mbaya, marubani wote waliona ndege mbele yao.
Unaambiwa aliekuepo chumba cha kuongozea ndege alikubali ombi la mmoja wa marubani kwenye ndege lililotaka ruhusa ya kutumia njia ya juu kwenye anga na akaruhusiwa lakini kumbe aliekua kwenye hicho chumba hakujua kwamba kuna ndege nyingine ambayo ilikua inatumia hiyo njia.
Baadae ndio muongozaji kwenye hiki chumba cha kuongozea ndege alishtuka ndio mipango ya kuziondoa hizi ndege kwenye njia moja ikaanza…. ilikua hekaheka ambapo walifanikiwa kuziokoa ndege kutogongana na zikakwepana kwa umbali mdogo sana.
Mara ya mwisho kwa ndege za Marekani kuponea chupuchupu kugongana zikiwa angani kama hivi ilikua ni mwaka 1978.








No comments:
Post a Comment