
Nigeria Super Eagles
Ushindi wa Super Eagles ya Nigeria ugenini dhidi ya Ethiopia umeipa matumaini ya kushiriki kombe lijalo la dunia.
Ethiopia ilipata goli la kuongoza kunako dakika ya 56 kupitia mchezaji Asefa.Bao hilo halikukaa kwa muda mrefu.kunako dakika ya 67 mkwaju uliopigwa na Emanuel Emenike uliishia langoni na kuwa 1-1.
Ethiopia watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kutumia nafasi kadhaa walizopata na pengine waliponea chupuchupu kunako dakika 77 ambapo mkwaju wa Nigeria ulirudishwa na mlingoti wa lango.
Goli la ushindi la Nigeria limepatikana kwenye dakika ya mwisho kwa njia ya penalty iliyofungwa kimiani na Emmanuel Emenike na kupalilia njia kwa bingwa hao wa Afrika ya kwenda Brazil.
Ivory Coast yapiga hatua kwenda Brazil

Didier Drogba
Ushindi wa Ivory Coast dhidi ya Senegal umekuwa hatua muhimu ya kuelekea katika fainali za kombe la dunia.
Mabao 3 yaliyofungwa na washambuliaji Didier
Drogba, Gervinho na Salomon Kalou yametosha kuiongezea matumaini Ivory
Coast ya kushiriki fanali za kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.Goli la kufutia machozi upande wa Senegal lilifungwa kimiani na mshambuliaji wa NewCastle Papiss Demba Cisse.
Mechi ya mkondo wa pili itachezwa mwezi ujao nchini Morocco kwa sababu Senegal inatumikia adhabu ya kutochezea kwenye uwanja wa nyumbani.
Burkinafaso 3 Algeria 2
Penalti ya dakika za mwisho iliyopewa Burkinafaso katika mazingira ya kutatanisha iliiwezesha timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Algeria.Hadi dakika ya 85 matokeo yalikuwa magoli 2-2 kabla ya Burkinafaso kupata penalti iliyowawezesha kuondoka na ushindi mdogo.
Ubegiji yakata tiketi ya Brazil

Timu ya taifa ya Ublgiji
Romelu Lukaku ameisaidia timu ya taifa ya Ubegiliji kufuzu kwenye fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil.
Magoli 2 yaliyotiwa kimiani na mshambuliaji huyo wa Chelsea yaliipatia ushindi Ubelgiji ikichezea ugenini dhidi ya Croatia.Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 25 sasa anaichezea Everton kwa mkopo kutoka Chelsea.
Alishinda magoli hayo katika kipindi cha kwanza,huku goli la kufutia machozi la Croatia likifungwa na Niko Kranjcar dakika chache kabla ya mechi kumalizika.
Timu ya taifa ya Ubelgiji inaongoza kundi A ikiwa na alama 25.inaizidi kwa alama 8 Croatia ambayo inashikilia nafasi ya pili.
Katika kundi B Italia imetoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Denmark ,lakini Italia imekwishafuzu.
Timu nyingine zilizofuzu ni Ujerumani,Uholanzi na Uswiss.Ugerumani katika kundi la C iliilaza Ireland magoli 3-0.Uholanzi iliinyeshea Hungary mabao 8-1 yakiwemo 3 yaliyofungwa na mahsmabuliaji wa Manchester United Robin Van Persie na Uswiss ikichezea ugenini iliifunga Albania mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment