
Ndege iliyokuwa imewabeba watu 20 imeanguka baada ya
kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja
wa ndege mjini Lagos.
Duru zinasema kuwa watu 8 wamefariki.Aidha ilikua inaelekea mjini Akure Kusini Magharibi mwa nchi, kwa mujibu wa msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani nchini humo.
Injini ya ndege ilikumbwa na hitilafu na kuisababisha ndege kuanguka na kuteketea.
Hata hivyo hakuna taarifa za kuthibitisha idadi ya watu waliofariki.
No comments:
Post a Comment