
Kocha
wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson anasisitiza kwamba
hafikiria na hana mpango wa kurejea katika shughuli za ukocha wa soka.
Manchester
United hivi sasa wanashikilia nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya England
chini ya uongozi wa David Moyes, aliyeshikilia nafasi hiyo baada ya
Ferguson kustaafu mwishoni mwa msimu uliopita.
"Mimi sina hamu ya kuwa meneja tena na kujisumbua roho yangu," alisema Ferguson.
"United wako mikononi mwa uongozi mzuri. David atakua vizuri tu. Ni meneja mzuri."
Ferguson, mwenye umri wa miaka 71, alidokeza kwamba Roman Abramovich alimtaka aiongoze Chelsea alipoinunua mnamo mwaka 2003.
"Walimtuma wakala aniulize Abramovich alipochukua madaraka kwa mara ya kwanza ya klabu hiyo lakini niliwaambia HAPANA."
No comments:
Post a Comment