
Al Liby alihusika na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi za Kenya na Tanzania mwaka 1998
Mwanamume raia wa Libya aliyekamatwa mapema mwezi huu
katika operesheni iliyofanywa na Marekani mjini Tripoli, amefikishwa
nchini Marekani kukabiliana na tuhuma dhidi yake.
Maafisa walisema kuwa Abu Anas al-Liby, ambaye
jina lake halisi ni, Nazih Abdul-Hamed al-Ruqai, alihojiwa akiwa kwenye
meli ya kijeshi ya Marekani kuelekea Marekani.Bwana Liby alisemekana kuwa na makosa ya kujibu mwaka 2000 katika mahakama moja mjini New York .
Mwendesha mashtaka mjini New York alisema kuwa Bwana Liby alihamishwa hadi katika kituo cha sharia mwishoni mwa wiki jana.
Atafikishwa mahakamani Jumanne.
Marekani ilikuwa inamsaka sana Anas al-Liby na alipokamatwa kuhusiana na operesheni iliyofanywa na wanajeshi wa Marekani tarehe 5 Oktoba, wengi waliona operesheni hiyo kama iliyokiuka uhuru wa libya.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ametetea hatua ya kukamatwa kwa Libya, akisema kuwa alikamatwa kihalali.
Serikali ya Libya imeitaka Marekani kuelezea kuhusu kukamatwa kwa Libya kiasi cha kumtaka balozi wa Marekani kufika mbele ya waziri wa sheria kufafanua kwa nini Liby alikamatwa.
No comments:
Post a Comment