
Kundi la Al Shabaab Somalia
Mwanamume anayeshukiwa kuwa mwanachama wa kundi la
kigaidi la Al Shabaab amefikishwa mahakamani nchini Kenya kwa tuhuma za
kuwasajili vijana wa Kenya kujiunga na kundi hilo nchini Somalia.
Mwanamume huyo kwa jina Aden Mohamed Maalim
mwenye umri wa miaka 38 kutoka nchini Somalia, alifikishwa mahakamani
pamoja na vijana wawili wanaoshukiwa kuwa ndio walikuwa wamesajiliwa
kujiunga na kundi hilo.Inaaminika kuwa walikuwa safarini kuelekea Somalia.
Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo aliamuru kuwa watatu hao waachiliwe kwa dhamana ya shilingi milioni mbili kila mmoja la sivyo wafungwe rumande hadi kesi yao itakaposikilizwa mwezi Februari mwaka ujao.
Juhudi za kupambana na ugaidi zimeshika kasi nchini Kenya hasa baada ya shambulizi la kigaidi dhidi ya jengo la kifahari la Westgate mjini Nairobi wiki tatu zilizopita kusababisha vifo vya zaidi ya watu sabini na kuwajeruhi mamia.
Kundi la kigaidi la Al Shabaab lilikiri kutekeleza shambulizi hilo na kusema kuwa lilikuwa linalipiza kisasi hatua ya Kenya kujihusisha na vita nchini Somalia.
Jeshi la Kenya likishirikiana na wanajeshi wa Somalia pamoja na wengine kutoka Afrika wamekuwa wakipambana na Al Shabaab kiasi cha kuwafurusha kutoka mji mkuu Mogadishu na kutoka maeneo ya Kismayo ambako walikuwa wanajikimu kwa kutumia bandari.
Kundi hilo sasa hufanya mashambulizi ya kuvizia.
Sasa wanamgambo hao wako maeneo ya vijijini ambako wangali wanadhibiti pakubwa
No comments:
Post a Comment