Sakata la klabu
ya Yanga kugomea kukubaliana na mkataba wa kati ya kamati ya Ligi na Azam Media
wa kuipa haki za matangazo ya televisheni ya mechi za ligi kuu kituo cha Azam TV
limechukua sura mpya baada ya Raisi wa shirikisho la soka la nchini TFF Leogdar
Tenga kuingilia kati.
Kwa
mujibu wa taarifa rasmi mtandao huu ulizozipata ni kwamba Tenga amewaandikia
barua Yanga akiwaambia kwamba amepata malalamiko yao dhidi ya mkataba wa
urushwaji wa matangazo ya mechi za ligi kupitia Azam TV.
Pia
Tenga amewaambia Yanga kwamba ameiomba kamati ya ligi kumpatia maelezo namna
mchakato mzima wa ugawaji wa tenda hiyo ulivyofanywa mpaka kufikia maamuzi ya
kuingia makubaliano na Azam TV.
Tenga
amewaomba Yanga kuwa wavumilivu ili kushughulikia malalamiko yao kuhakikisha
muafaka unafikiwa kwa ajili ya manufaa ya soka la Tanzania.
No comments:
Post a Comment