Kenya itakuwa
nchi ya 100 ya kigeni kuwa na mchezaji anayekipiga kwenye ligi kuu ya England
wakati kiungo wa kimataifa wa nchi hiyo Victor Wanyama atakapocheza mechi yake
ya kwanza akiwa na Southampton.
Na yote haya
yasingewezekana kama isingekuwa kwa mama wa watoto sita, ambaye ametumia maisha
yake yote akifanya kazi ya mkuu wa kitengo cha michezo katika shule moja jijini
Nairobi.
Wanyama, 22,
alianza kufahamika vizuri kwenye ulimwengu wa kimataifa wa soka mwezi November
mwaka jana wakati alipofunga goli katika mechi kati ya klabu yake ya zamani na
FC Barcelona na kuisadia klabu hiyo ya Uskochi kushinda 2-1 katika mechi ya
makundi ya Champions League.
Kiungo huyo
mwenye kimo cha 6ft 2in anayecheza kiungo cha ulinzi alivivutia vilabu vya
Manchester United, Arsenal na Everton miongoni mwa vingine vingi lakini hatimaye
mwishoni alisaini kuichezea Southampton kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya
klabu hiyo £12.5million wakati wa dirisha la usajili hili
lilipofunguliwa.
![]() |
| Sehemu wanazotoka wachezaji wanaokipiga kwenye EPL |
Wachezaji kutoka
Albania mpaka Zimbabwe na nchi zingine 98, ukiachana na mataifa manne yaliyomo
ndani ya ya mipaka ya UK, yameshakuwa na wawakilishi katika misimu 21 tangu
ulipoanzishwa rasmi mfumo wa Premier League mnamo 1992 - lakini Wanyama anakuwa
mchezaji wa kwanza kuiwakilisha nchi yake ya Kenya.
Akiwa na miaka 22
sasa lakini tayari ameshachezea vilabu vya juu kwa maana ya professional clubs
katika nchi tano tofauti, kuanzia AFC Leopards ya nyumbani kwao akiwa na miaka
15, akaenda Helsingborgs huko Sweden akiwa na miaka 16, Beerschot ya Belgium
akiwa na miaka 17, Celtic ya Scotland akiwa na miaka 20 na sasa yupo
Southampton.

Lakini bila
uangalizi na kujitoa kwa mwalimu wa michezo Sophie Makoba, 48, ingekuwa vigumu
kwa Wanyama kutambua na kukiendeleza kipaji chake.
Kwa msaada wake,
Wanyama aliweza kujiendeleza na kuwa mtu muhimu katika nchi yenye wakazi 44
million kwa kuwa mkenya wa kwanza kucheza kwenye ligi kuu ya England.
'Premier League
ni ligi bora na ndio inayofuatiliwa kwa kiasi kikubwa nchini Kenya na najua
watapata mashabiki wengi sasa hivi wakiwa wamemsajili Victor,' alisema Makoba
katika mahojiano na gazeti la Daily mail.
'Watu wa Kenya
wana shauku kubwa ya msimu mpya wa EPL. Watu wengi wanaangalia mechi za EPL japo
sio wote wanaoweza kuangalia kwenye TV zao kwa sababu ni gharama kubwa
kulipia.'
Akiwa bado mdogo
Wanyama alikuwa na bahati nzuri ya kujiunga na shule ya sekondari - Kamukunji
High School, ambapo mwalimu amekuwa akifanya kazi. "Hakuwa na akili sana
darasani lakini ndio mchezaji mzuri zaidi kiwanjani, aliweza kupata nafasi
kwenye timu ya kwanza ya shule akiwa amezidiwa na wenzie umri wa miaka mitatu
alipokuwa na miaka 13,' anaelezea
mwalimu Makoba.
Makoba alikuwa
mwanamichezo wa kweli, aliwahi kucheza michezo ya gymnastic akiwa mdogo na pia
akajaribu kucheza netball na riadha kabla ya hajaenda kucheza basketball katika
ngazi ya taifa.
Angeweza
kuendelea na michezo lakini kwake elimu ilikuwa ni bora zaidi, na hivyo
alipopata nafasi ya kusoma chuo akaamua kuachana na micheoz na kujiunga na chuo.
'Wakati
nilipomaliza chuo mwaka 1990, nilikuwa nina miaka 25 na nikaamua kufanya kazi
katika shule ya Kamukunji kama mkuu wa kitengo cha michezo shuleni. 'Niliona
kwamba kuna wanafunzi ambao hawakuwa vizuri kimasomo darasani ambao wangeweza
kupata mafanikio kupitia michezo na kuanzia hapo tukaanza kitu ambacho kimekuwa
utamaduni wa kuendeleza michezo mashuleni.'
Kamukunji
hakukuwa na mazingira mazuri. Ilikuwa ni kama shule nyingine tu za kawaida
jijini Nairobi, ambapo wananchi wa maisha ya kawaida ambao wana uwezo wa kupata
kiasi kisichozidi £1,000 kwa mwaka na pia vifaa vya ufundishaji shuleni hapo
vilikuwa vya kawaida.
Makoba amekuwa
mpenzi mkubwa wa soka kwa muda mrefu sana. Anaisapoti klabu ya Manchester United
na wachezaji kama George Best, Robin van Persie ndio anawapenda lakini Roy
Keane ndio zaidi.
Familia yake yote
inapenda soka. Mumewe ni shabiki mkubwa wa Arsenal, watoto wake wawili wa kiume
wote wanashabiki a Man united kama mama yao, lakini mtoto mwingine wa kiume yeye
ni shabiki wa Chelsea.
Pamoja na kuwa na
mapenzi na mchezo lakini Kenya haina vifaa vizuri vya michezo.
'Hatukuwa na
uwanja pale Kamukunji hivyo nilikuwa naandaa mpango timu yangu kufanya mazoezi
katika uwanja wa kuazima uliopo karibu na shule,' alisema Makoba. 'Uwanja wa
kuazima ulikuwa unatumika jioni hivyo ilitubidi kuanza mapema, kabla ya wenye
uwanja wenyewe hawajafika. Hivyo tulipendelea kufanya mazoezi asubuhi alfajiri
mpaka kulipokucha kwa ajili ya watoto kurudi shule.'
Kujitoa kwa
Makoba kulianza kulipa miaka 15 baadae wakati Kamukunji ilipoanza kukuza vipaji
vya makinda ambao walienda kupata nafasi kwenye vilabu barani ulaya katika ligi
tofauti.
Baadhi ya vipaji
vilivyokuzwa katika shule ya Kamukunji chini ya uangalizi wa Makoba, miongoni
mwao ni mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya Dennis Oliech, 28, anayekipiga
Ajaccio inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa, mshambuliaji mwingine Patrick Oboya,
26, ambaye amewahi kuchezea vilabu tofauti nchini Czech Republic na Slovakia,
pia wapo wachezaji wanaokipiga kwenye ligi ya nyumbani kama Kevin Ochieng, winga
ambaye ameshavichezea vilabu kadhaa vya Kenya.
Bila shaka majina
makubwa katika soka la Kenya kwa hivi sasa ni Wanyama na kaka yake McDonald
Mariga Wanyama, 26, kiungo wa ulinzi wa Inter Milan ambaye kwa sasa yupo kwa
mkopo Parma.
Mariga angeweza
kuwa mkenya wa kwanza kucheza katika ligi kuu ya England mnamo mwaka 2010,
wakati Roberto Mancini alipojaribu kumnunua kwenda Manchester City, lakini
alikosa kibali cha kufanya kazi nchini humo.
Japo suala hilo
liliingiliwa kati na waziri mkuu wa Kenya wa wakati huo Raila Odinga, ambaye
alitumia masaa kadhaa kuzungumza na waziri mkuu Gordon Brown na maofisa wengine,
lakini ilishindikana kumpatia Mariga kibali.
'Siku zote
niliamini Victor angeenda mbali,' anasema Makoba. 'Mara zote amekuwa mtaratibu,
mpole na mwenye heshima. Mama yake Mildread na baba, Noah, walikuwa wakifanya
kazi kwenye shirika la reli la Kenya wakati Victor akiwa
mdogo.
Walikuwa maskini,
wakiishi na watoto nane katika nyumba ndogo sana. Mildred anaishi kwenye nyumba
nzuri sana, kwenye eneo zuri. Wanaendesha magari mazuri kama Hummer na Cadillac.
Nina furaha sana na mafanikio ya vijana wangu.'
Makoba alihama
kutoka Kamajunji mwaka jana na kuhamia kwenye shule ya wasichana watupu, ambapo
jukumu lake ni kuendeleza vipaji vya soka na basketball kwenye shule.



No comments:
Post a Comment