Kulia
ni mtoto aliyebakwa na baba yake kisha kuzalishwa akiwa na mtoto wake
wakati wakitoka mahakamani. Kushoto ni mama mzazi wa binti aliyebakwa na
kuzalishwa.
MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa
Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na
kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka 15( jina linahifadhiwa).
Mwendesha mashitaka wa serikali Archiles Mulisa aliiambia mahakamani
hiyo Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo ni Yusufu Amani
(39) anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya
kutengana na mkewe.
Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 sura
ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, pamoja na kifungu cha
158(a) cha makosa ya kuzini.
Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza
kujihusisha kimapenzi na mwanaye Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe
ambapo Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.
Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa miaka 12 na
alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la Tano jambo ambalo wamedumu
nalo kwa miaka minne hadi ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito
Mei, 2012.
Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti asitoe taarifa kwa
mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito alimwambia
amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.
Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa kutokana na
ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti pamoja na ushahidi wa
kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kupima Vinasaba
kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa ulidai kuwa Mshtakiwa
ndiye baba halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15 ya vipimo vya Vinasaba
kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa asilimia 99.9.
Aidha kabla ya kutoa hukumu, Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea
ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini hali ikawa
tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote
itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya hukumu.
Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo alimhukumu kwenda jela
miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu endapo
hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo, Mtuhumiwa huyo alidai kuwa
hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na Mkewe ambaye aliapa
kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume mwingine jambo ambalo
lilipingwa vikali na hakimu na kudai kuwa “mfa maji haachi kutapatapa”
No comments:
Post a Comment