
Watu tisa, wawili kati yao wakiwa polisi wa Kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam wamekamatwa wilayani Kisarawe, mkoani Pwani kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha meno 70 ya tembo (kilo 305) kinyume na sheria.
Meno hayo kwa hesabu za kawaida ni sawa na tembo 35, wameuawa na kwamba thamani yake ni zaidi ya Sh850 milioni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei,
alisema watuhumiwa hao walikamatwa Kisarawe usiku wa kuamkia jana na
askari wa wanyamapori waliokuwa kwenye operesheni.
Matei alisema watuhumiwa walikamatwa kwenye
kizuizi cha Kauzeni, Kata ya Vikumburu, Tarafa ya Chole na kwamba,
walikuwa wakisafirisha meno hayo kwa kutumia gari aina ya Toyota Surf
kwenda Dar es Salaam.
“Ni kweli wamekamatwa watu tisa, wawili wakiwa ni
Polisi wa Oysterbay, nimepata hiyo taarifa na nimeshamtuma Ofisa
Upelelezi Mkoa (RCO) kuwaleta Kibaha,” alisema Matei.
Kamanda Matei alitaja watuhumiwa kuwa ni mkazi wa
Tandika Yombo, mkazi wa Kinondoni Studio, mkazi wa Tandika hewa, mkazi
wa Mbagala Charambe na mkazi wa Chanika. Pia, polisi wawili wanaodaiwa
wa Kituo cha Oysterbay.
Wakati polisi hao wakikamatwa, Idara ya Magereza
imetangaza kuwafukuza askari wanne wanaodaiwa kukamatwa wakiwa wamepakia
meno ya tembo Julai 23, mwaka huu.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja,
aliwataja waliofukuzwa kuwa ni Mrakibu Msaidizi, Joseph Kimaro, Sajenti
Ketto Ramadhan, Koplo Silyvester Dionice na Wada Richard Barick.
Minja alisema askari watatu waliohusika
wamefukuzwa kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Magereza,
watafikishwa mahakamani baada ya polisi kukamilisha uchunguzi.
Alisema Mkuu wa Gereza la Kiteto, Mrakibu Ally
Sauko, amevuliwa uongozi na kuhamishiwa Ofisi ya Mkuu wa Magereza
Manyara, akisubiri uamuzi wa mamlaka.
ya Nidhamu,” alisema Minja.
No comments:
Post a Comment