Daladala lenye namba za usajili T 741 AEG baada ya kuhama njia na kuparamia mtaro uliopo jirani na bucha eneo la Mwenge. |
Daladala lenye namba za usajili T 741 AEG linalofanya safari zake kati ya Temeke na Mwenge asubuhi hii nusura liingie katika bucha iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar katika barabara iendayo Afrika Sana. |
Daladala hilo lilisaidiwa na mtaro uliopo mbele ya bucha hiyo baada ya dereva wake kushindwa kuliongoza na kuhama barabara. |
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio, daladala hilo halikuwa na abiria na hakuna mtu aliyejeruhiwa.
No comments:
Post a Comment