
CHRISTIAN BENTEKE ameiweka Aston Villa kwenye wakati mgumu sana baada ya kuomba rasmi kimaandishi kwamba anataka kuondoka kwenye klabu hiyo.
Chelsea na Spurs sasa zitapigana vikumbo kusaka saini ya mshambuliaji huyo ambaye anatajwa kuwa na thamani isiyozidi £30million baada ya klabu ya Aston Villa wenyewe kuthibitisha kwamba wakipata ofa nzuri watamuuza mshambuliaji huyo.
Benteke, 22, hakuwepo kwenye kikosi cha Villa kilichosafiri kwenda Ujerumani kwa jili ya maandalizi ya msimu mpya.
Kwenye taarifa rasmi, Villa ilisema: “Tumemtaarifu Christian kwamba ikiwa tutapokea ofa nzuri wakati huu wa pre-season ambayo itakuwa inaendana na hesabu zetu - then tutamuuza.
“Lakini ataendelea kuwa mchezaji Villa ikiwa hilo halitotokea."Jose Mourinho na Andre Villa Boas ndio makocha wanaonekana kummezea mate mbelgiji huyo ingawa Arsenal nao wanaweza kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kushindana kupata saini ya mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment