
Mahakama ya rufaa nchini Misri imeamuru kuachiliwa
huru kwa wanawake, 21 wakiwemo wasichana saba waliofungwa jela mwezi
jana kwa kuandaa maandamano ya kumuunga mkono aliyekuwa Rais Mohammed
Morsi.
Watoto hao wamepewa kifungo cha nje cha miezi
mitatu. Mahakama hiyo pia ilipunguza kifungo cha miaka 11 walichokuwa
wamepewa wanawake hao 14.Hata hivyo makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa hukumu hiyo.
Mmoja wa wanaharakati hao walitaja hukumu hiyo kama ya wazimu.
Wanawake hao walifikishwa mahakamani wakiwa wamevalia nguo nyeupe huku wakiwa wamebeba maua ya waridi.
Aidha wanawake hao na watoto walishiriki maandamano ya kumuunga mkono aliyekuwa rais Morsi na jamaa zao wanasema ni maandamano ya kwanza waliyowahi kushiriki na kuyaendesha bila vurugu.
Mamia ya watu wameuawa nchini Misri tangu hatua ya kumwondoa Morsi mamlakani mwezi Julai kusababisha maandamano na vurugu nyingi.
No comments:
Post a Comment