Dalili za kukaribia kushindwa kwa waasi wa M23 nchini
DRC, ni ishara ya mabadiliko ya kisiasa na mpangilio wa kijeshi ambayo
yanaweka wazi matumaini ya amani katika nchi hiyo kubwa na ambayo
imekuwa na migogoro kwa miaka mingi.
Waasi wa M23 Mashariki mwa nchi, wamepata pigo
kubwa katika wiki chache zilizopita , na kulazimisha kiongozi wao
Bertrand Bisimwa kutoa amri ya kusitisha vita na kutaka mazungumzo ya
amani kuanza tena nchini Uganda.Hasa baada ya vita hivyo kuendelea kwa miongo miwili.
"Kundi la M23 limekuwa kundi ambalo harakati zake zimekuwa wazi sana Mashariki mwa nchi. Kushindwa kwake haimaanishi ndio mwisho wa vita na mwanzo wa amani. Ni mapema mno kutabiri hilo,’’ alisema Stephanie Wolters kutoka katika taasisi ya mafunzo ya usalama nchini Afrika Kusini.Ili Kuelewa matumaini ya hatimaye kumalizika kwa vita yanatokana na nini, ni muhimu kuelewa ambavyo waasi wa M23 wamekuwa wakiendesha harakati zao na ambavyo walifurushwa kutoka katika ngome zao.
Wakati waasi wa M23 walidhibiti mji wa Goma - Novemba 2012, lilikuwa jambo la aibu sana kwa serikali ya Rais Joseph Kabila pamoja na kushinikiza jamii ya kimataifa kuchukua hatua baada ya madai ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu kuibuka.
Rais Kabila alifanyia jeshi mabadiliko na dalili ya kuonyesha mambo yalikuwa yanakwenda vyema, sababu hakuna madai zaidi ya ukiukwaji wa haki za bindamau yaliwahi kusikika.
Machi mwaka huu, Umoja wa Mataifa iliidhinisha kikosi cha wanajeshi 3,000 wa Afrika waliokuwa na jukumu la kupambana na waasi.
Wanajeshi hawa wamekuwa wakitumia ndege za helikopta kushambulia maeneo ya waasi wakisadiana na wanajeshi wa UN (Monusco)ambao tayari walikuwa wanakabiliana na waasi hao .
Congo na Rwanda: Majirani mahasimu
Kwa sasa kuna taarifa kuwa wanajeshi wa UN watapokea ndege zisizo na rubani, ili kufanyia uchunguzi waasi hao na ambavyo wanaendesha harakati zao.Umoja wa mataifa umetuhumu Rwanda na Uganda kwa kuunga mkono waasi wa M23. Hata hivyo, nchi hizo zimekanusha madai hayo.

Mazungumzo ya amani kati ya viongozi wa M23 na Serikali ya DRC yalifanyika mjini Kampala Uganda
Marekani imesitisha msaada kwa Rwanda, baada ya kuituhumu kusaidia waasi wa M23 kupiga serikali ya DRC na ambao wanaaminika kutumia watoto kama wapiganaji wa kundi hilo.
Ni mapema sana kusema kuwa kundi la waasi wa M23 limeshindwa.
Kwa miaka mingi serikali ya DRC imeshindwa kupambana vilivyo na makundi ya waasi Mashariki mwa nchi, sababu moja ya hilo ni washirika wa kimataifa kujihusisha na vita hivyo.
Serikali ya Rais Kagame imesisitiza kuwa ilituma wanajeshi wake kusaidia serikali ya DRC kupambana na waasi wa FDLR, kundi la waasi wa kihutu waliohusishwa na mauaji ya kimbare ya Rwanda na ambalo linapinga ushawishi wa watutsi katika eneo hilo.
Jambo ambao wadadisi wanasema ni kwamba lazima serikali ya DRC iwe na mpango maalum wa kusuluhisha tatizo la uasi katika eneo hilo la sivyo makundi ya waasi kama FDLR ambayo yako kimya huenda yakarejea tena kuisumbua nchi hiyo baada ya M23 kuzimwa.
No comments:
Post a Comment