
SUPASTAA, Gareth Bale, amefichua kwamba alimtwangia simu staa David Beckham kuomba ushauri kabla ya kuchukua uamuzi wa kujiunga na Real Madrid katika usajili uliopita wa majira ya kiangazi.
Staa huyo wa kimataifa wa Wales alivunja rekodi ya
Cristiano Ronaldo ya uhamisho baada ya kujiunga na Los Blancos kwa ada
ya Pauni 86 milioni Septemba mwaka huu.
Winga huyo wa zamani wa Tottenham Hotspurs,
alisema alipata ushauri kutoka kwa Beckham aliyewahi kung’ara na timu
hiyo ya Hispania na alimfundisha namna ya kuhimili maisha ya Hispania.
Alipoulizwa ni wachezaji gani amekuwa akiwasiliana
nao, Bale alisema: “Wote. David Beckham alinitumia meseji ya kunitakia
heri na mambo mengine. Lilikuwa jambo zuri sana na nimefurahi.
“Alifanya mazoezi Tottenham tukiwa pamoja kwa muda
fulani, hivyo namfahamu vizuri na nimekuwa nikimtumia meseji na
kumpigia simu.
“Namfahamu Jonathan Woodgate pia na nimekuwa
nikifanya naye mawasiliano. Nilikutana pia na Steve McManaman kwenye
mahojiano na tulizungumza mengi sana.”
No comments:
Post a Comment