
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo unasema unasikitika kuwa watu waliofanya ukatili
katika mji wa Minova mwaka jana hawakufikishwa mahakamani.
Umoja wa Mataifa unasema una ushahidi wa kesi
135 za ubakaji pamoja na mauaji na wizi wa ngawira uliofanywa katika
eneo la Minova mwezi Novemba mwaka jana.Ulilishutumu jeshi la Congo kufanya uhalifu huo.
Inaarifiwa maafisa 12 wa jeshi la Congo walisimamishwa kazi kwa muda, lakini Umoja wa Mataifa unasema hakuna aliyefikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment