HAJAWAHI kukosea ndani na nje ya uwanja. Baada ya penzi lake la
mkewe, Bia Anthony, kufa Desemba mwaka jana, mkongwe wa soka nchini
Brazil, Ronaldo de Lima, ameibuka kivingine kabisa.
Ronaldo ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na DJ
mrembo, Paula Morais, ambapo penzi lao linaonekana kushika chati nchini
Brazil kama ilivyo ada kwa Ronaldo ambaye ni maarufu nchini humo.
Staa huyo wa zamani wa Barcelona, Inter Milan,
Real Madrid na AC Milan, ameachana na mkewe aliyedumu naye kwa miaka
saba na sasa inaonekana amezama katika penzi la Paula kiasi cha
kufuatana naye kila mahali.
Penzi lao lilianza kudhihirika katika tamasha la
Samba nchini Brazil hivi karibuni ambapo wawili hao walijitokeza
hadharani na kuvutia umati wa mashabiki.
Kama vile haitoshi, Paula alitoa kiashirio kwamba
yuko katika penzi zito na Ronaldo na kwamba anaiangalia afya ya nyota
huyo kwa karibu hasa baada ya staa huyo kupunguza kilo 17 akifuata
mpangilio wa vyakula kwa mujibu wa kituo kimoja cha televisheni nchini
Brazil.
Paula alituma picha ya Ronaldo akiwa ameshikilia
kikaangio kilichokuwa na mayai ya kukaanga huku akiandika ‘Jiko ni
sehemu ya Mwanamume, nakupenda.’
Kama vile haitoshi, siku za karibuni Ronaldo
alisafiri na Paula mpaka nchini Hispania kwa ajili ya kula raha katika
miji mbalimbali nchini humo. Walionekana wakiwa katika fukwe za maraha
za Ibiza wakiponda starehe.
Pia walionekana wameshikana mikono katika Jiji la
Madrid wakiwa katika maduka ya Chanel & Hermes wakifanya manunuzi
huku wakipiga stori za mahaba.
Kama inavyoonekana pichani, Ronaldo pia amekuwa
akiwa sambamba na Paula hadi katika sehemu yake ya kazi huku akivamia
katika chumba cha MaDJ ambacho ni maalumu kwa wapiga muziki peke yao.
Huu ni mwendelezo wa Ronaldo katika harakati zake
za kupenda vimwana ambapo penzi lake la awali na mkewe Bia, liliingia
katika dosari baada ya Ronaldo kukumbwa na kashfa ya kuingia chumbani na
wanaume wanne waliojibadili jinsia. Hata hivyo ndoa yao baadaye
iliendelea baada ya Ronaldo kuomba msamaha.
Mtoto wao wa kwanza, Maria Sophia, alizaliwa
Desemba 24, 2008. Mtoto wa pili, Maria Beatriz alizaliwa Aprili, 6 2010
na Mtoto wao wa tatu aliyepewa jina la Maria Alice, alizaliwa miaka 10
kamili tangu Ronaldo apate mtoto wake wa kwanza wa kiume.
Ronaldo ambaye pia alizaa na mkewe wa kwanza, Milene Domingues, Aprili 6, 2000. Ndoa yao ilidumu kwa kipindi cha miaka minne tu baada ya Milene kugundua tabia za kifuska za Ronaldo.

Ronaldo ambaye pia alizaa na mkewe wa kwanza, Milene Domingues, Aprili 6, 2000. Ndoa yao ilidumu kwa kipindi cha miaka minne tu baada ya Milene kugundua tabia za kifuska za Ronaldo.
Kabla ya hapo, Ronaldo alikuwa katika uhusiano
mzito wa kimapenzi na mwanamitindo mrembo mwigizaji, Susana Werner,
ambaye alikutana naye mwaka 1997 kabla ya kuwa naye katika uhusiano wa
muda mrefu kiasi cha kwenda kuishi naye jijini Milan wakati akiichezea
Inter Milan.
Ronaldo pia aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi
na mwanamitindo maarufu wa Brazil, Daniela Cicarelli, ambaye alimpatia
mimba lakini ikatoka.
Uhusiano wake na mrembo huyu ulidumu kwa miezi
mitatu tu licha ya Ronaldo kumvalisha pete ya uchumba katika ukumbi wa
kifahari Chateau de Chantilly ambapo gharama za tukio hilo liligharimu
kiasi cha Pauni 700,000.
Desemba mwaka huo, Ronaldo alifanya vipimo vya DNA
na kuthibitisha kwamba alikuwa baba wa mtoto, Alexander, aliyezaliwa
Aprili 2005.
Mtoto huyo alitokana na uhusiano wa muda mfupi
kati ya Ronaldo na Michele Umezu ambaye ni mhudumu wa baa na walikutana
kwa mara ya kwanza jijini Tokyo katika fainali za Kombe la Dunia mwaka
2002.
Baadaye Ronaldo alikiri kwamba alikuwa anataka
kufunga uzazi kwa madai kwamba watoto wanne walikuwa wanamtosha, lakini
hapo hapo akajikuta akipata mtoto wa tano na Bia ambaye alikuwa wa tatu
kwao.
Kwa sasa Ronaldo anatarajiwa kuwa bize na shughuli
za maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika
nchini kwao Brazil Juni mwakani huku akiwa amechaguliwa kuwa miongoni
mwa mabosi wa shughuli yenyewe.
Ronaldo pia anatazamiwa kuwa Rais wa Shirikisho la
Soka la Brazil baada ya kuondoka madarakani kwa Rais wa sasa, Ricardo
Teixeira, mwakani.
No comments:
Post a Comment