
Jeshi la Jamhuri ya Demokrasi ya Congo linasema
limeikomboa miji miwili mengine kutoka kwa wapiganaji wa M23, karibu na
mpaka wa Rwanda.
Jeshi liliwaambia waandishi wa habari kwamba
Jumapili limeteka Rutshuru na Kiwanja, katika jimbo la Kivu kaskazini;
baada ya kuteka Kibumba Jumamosi.Umoja wa Mataifa unasema mwanajeshi mmoja wa Tanzania, katika kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, aliuwawa Kiwanja, akijaribu kuwalinda raia.
Mapigano yalizuka Ijumaa, siku chache baada ya mazungumzo ya amani ya mjini Kampala, Uganda, kuvunjika..
No comments:
Post a Comment