
Boateng hucheza soka ya kulipwa Ujerumani
Mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya
Ghana, Kevin-Prince Boateng atakosa mechi ya mkondo wa kwanza ya
kujitafutia nafasi kwenye dimba la kombe la dunia dhidi ya Misri,
kutokana na jeraha la goti.
Mechi hiyo itachezwa mjini KumasiNa baada ya kufanyiwa ukaguzi na madakatri, imegunduliwa kuwa Boateng lazima afanyiwe upasuaji kwenye goti lake la kushoto.
Kocha wa timu ya Black Stars, Kwesi Appiah, ameamua kutafuta mchezaji mwingine kuchukua nafasi ya Boateng.
Mechi za mkondo wa pili za kufuzu kwa kombe la dunia litakalochezwa nchini Brazil mwaka ujao, zitachezwa mjini Cairo, Misri tarehe 19 Novemba.
Hata hivyo, Ghana wameomba michuano hiyo kuhamishiwa kwingineko kwa sababu za usalama kufuatia hali ilivyo nchini Misri.
No comments:
Post a Comment