Watoto katika wilaya ya Makoko lazima wajifunze kuogelea ikiwa
wanataka kwenda shuleni. Kwa sababu wilaya hiyo katikati mwa mji mkuu wa
Nigeria Lagos imekumbwa na mafuriko tangu mwezi Machi 2013. Shule
inayoelea ni mfano wa usanifu majengo wa kiafrika "Afritecture". Usanifu
huu unaweka kando dhana za ujenzi wa kimagharibi na kutegemea zaidi
mbinu za kienyeji na vifaa kama vile mbao.
No comments:
Post a Comment