
Viongozi wa dunia wamekuwa akitofautiana kujhusu hatua za kuchukua dhidi
ya Serikali ya Assad kwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia
Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanajiandaa kurejea
nchini Syria kuendelea na uchunguzi kuhusu ikiwa silaha za kemikali
zilitumika katika miji mingine ya nchi hiyo mbali na Damascus
Wachunguzi hao tayari wamethibitisha kuwa gesi
ya sumu aina ya Sarin, ilitumika katika kuwashambulia watu katika
kitongoji kimoja cha Damascus mwezi Agosti tarehe 21 ambapo mamia
waliuawa.Sasa wanajiandaa kutembelea maeneo mengine matatu ambako inaaminika silaha za sumu zilitumika ingawa kwa kiwango kidogo mapema mwaka huu. Shambulizi lilifanyika katika eneo la Aleppo,mjini Homs na karibu na Damascus.
Serikali ya Syria pamoja na waasi zinatuhumiana kwa kufanya mashambulizi .Wachunguzi hao wataamua ikiwa silaha za kemikali zilitumika lakini hawatasema ni nani wa kulaumiwa.
No comments:
Post a Comment