Siasa zimechemsha Ujerumani ambapo viongozi wa vyama mashuhuri vya
kisiasa wa chama cha Free Democratic FDP wamejiuzulu na uongozi mzima wa
chama cha Kijani kujizulu baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi.
Kiongozi wa chama cha FDP Phillip Rösler ametangaza kujiuzulu hapo
Jumatatu baada ya chama chake kushindwa vibaya kuwahi kushuhudiwa kabla
katika uchaguzi wa Ujerumani uliofanyika Jumapili na kusababisha
kuenguliwa kwa chama hicho katika bunge la Shirikisho la Jamhuri ya
Ujerumani.Rösler Naibu Kansela anayemaliza muda wake ambaye amejiuzulu kama kiongozi wa chama hicho chenye kupendelea wafanya biashara na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ni miongoni mwa mawaziri waliopoteza viti vyao katika uchaguzi huo ambapo chama chao kimeboronga vibaya.
Rösler mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikuwa pia waziri wa uchumi katika serikali ya Merkel amesema wakati akijiuzulu kwamba huko ni kushindwa vibaya kabisa kwa chama hicho kuwahi kushuhudiwa katika historia.

Chama cha FDP ambacho mara nyingi kimekuwa kikishiriki katika serikali kama mshirika mdogo kuliko chama chengine chochote kile cha Ujerumani tokea kilipochaguliwa mara ya kwanza hapo mwaka 1949 kimeshindwa kujipatia asilimia tano ya kura ili kuweza kubakia bungeni.
Rösler na mgombea mkuu wa chama hicho Rainer Brüderle mwenye umri wa miaka 68 aliyeonekana kuwa na huzuni kubwa wote walikuwa tayari wametangaza hapo Jumapili kwamba watawajibika kisiasa kufuatia matokeo hayo ya uchaguzi.
Matumaini mapya ya FDP

Lindner yumkini akachaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama hicho katika mkutano mkuu wa chama utakaofanyika baadae mwaka huu na ameahidi hapo Jumatatu atapigania kurudisha heshima ya chama hicho.
Chama cha FDP ambapo wafuasi wake wanajulikana kama Waliberali pole pole kimekuwa kikibadili mwelekeo wake tokea kumalizika kwa Vita Baridi kutoka kuwa uliberali wa kisiasa hadi utetezi wa uhuru wa watu binafsi hadi kuwa uliberali wa kiuchumi na utetezi wa ubepari wenye kutegemea uhuru wa masoko.
Katika kipindi cha miaka minne iliopita chama hicho kimekuwa kwenye mfarakano wa ndani ya chama jambo ambalo linatajwa kuwa ndio lililosababisha kuanguka kwa chama hicho kwenye uchaguzi kutoka asilimia 10 iliokuwa ikishikilia tokea uchaguzi wa mwaka 2009 hadi kuwa asilimia 4.8 katika uchaguzi huu.
Uongozi mzima kujiuzulu

Akitangaza uamuzi huo Jumatatu Roth pia amesisitiza kwamba iwapo Kansela Angela Merkel atapendekeza kuunda serikali ya mseto na chama hicho pendekezo hilo linapaswa kuzingatiwa.
Kwa hivi sasa Merkel amewasiliana na chama kikuu cha upinzani SPD kupendekeza kile kinachojulikana kama serikali ya "muungano mkuu" na chama hicho.
No comments:
Post a Comment