
TAARIFA
mbalimbali zilizowahi kutolewa na mwigizaji na mwanamuziki maarufu
nchini, Zuwena Mohamed 'Shilole' kuhusu uhalisia wa maisha yake
zimeelezwa kuwa si za kweli, kwa mujibu wa watu wa karibu na staa huyo.
Shilole
aliwahi kuliambia gazeti moja mwaka huu lililofanya
naye mahojiano kuwa mtoto wake wa kwanza mwenye umri wa miaka 10
alijifungua baada ya kubakwa na baba wa mtoto huyo ambaye amedai kuwa
wawili hao walishaishi kama mke na mume kwenye nyumba ya familia ya mume
huko Igunga, Tabora.
"Shilole nilijuana naye tangu mwaka 2000, kwa wakati huo alikuwa amemaliza darasa la saba.
Ukweli
ni kwamba wote tulikuwa watoto, mwenzangu hakuwa na uangalizi wa karibu
na familia yake kwani alikuwa hana wazazi nami pia nilikuwa sina wazazi
bali nilikuwa na dada mmoja tu, tulianza kuishi pamoja katika nyumba ya
familia," anaanza kwa kusema Makala Joseph mwanamume aliyezaa na
Shilole mtoto wa kwanza.
Anasema
licha ya kwamba alimkana, akamkimbia, akamsusia mtoto na baadaye akaja
kumwiba kwa siri, lakini bado anampenda na kumsihi kama atarudisha moyo
wake yupo tayari kumpokea kama mkewe, kwani bado hajaoa akimsubiri
Shilole.
Makala
ambaye sasa anaishi Igunga mkoani Tabora akifanya kazi ya utingo,
anasema kauli ya staa huyo ina athari kubwa kwa mtoto ambaye sasa bado
ni mdogo.
"Unaposema
kuwa ulibakwa haileti picha na mtazamo mzuri kwa watu, hata hivyo kwa
mtoto pia ina athari kubwa, anakua na itafikia kipindi atataka kujua
ukweli wa maisha ya mama yake, atakaposikia mama yake alibakwa italeta
picha gani?
"Tulikubaliana
mpaka tukaishi miaka miwili na kuzaa mtoto ambaye mwenzangu alikimbia
na kuniachia mtoto akiwa na miezi mitano mara baada ya kukutana na
dereva wa magari makubwa na si kwamba nilimbaka, kama ni hivyo kwanini
asingeenda mahakamani na kufungua kesi?" Alihoji Makala.
Anasema
ingawa anamtunzia mtoto wake, si vema kwa Shilole kuzungumza kauli
zisizo za kweli na kuficha ukweli, huku akiwapakazia watu wengine kesi
zisizo kweli.
"Leo ananiona mimi mshamba. Sawa lakini akumbuke kuwa alitoka huku ni vema kuheshimu sehemu uliyotoka kuliko kuleta dharau.
Mimi
si msemaji ila tu nimechoshwa na kauli zake, kila siku kwenye magazeti
eti alibakwa huku mtuhumiwa nipo kwanini asingeshtaki, hakuna asiyejua
hapa Igunga kama niliishi naye kama mke wangu.
"Wakati huo mimi nilikuwa utingo na yeye alikuwa akiuza nyanya sokoni.
Maisha yaliendelea hivyo mpaka alipokuja kupata ujauzito na baadaye alijifungua.
Ila
nyongo ilitumbukia baada ya yeye kukutana na huyo bwana ambaye
alimshawishi akimbie kwangu na akaenda kumzalisha huko Dar es Salaam."
Kauli
ya Makala inafafanuliwa zaidi na dada yake Sara Joseph ambaye ndiye
wifi wa Shilole: "Ni kweli yeye hana wazazi kama anavyoeleza katika
mahojiano yake kwenye magazeti, redioni na runinga.
Lakini
kuna baadhi ya mambo anayoyasema si ya kweli. Angezungumzia maisha yake
halisi mimi sina neno, adanganye anavyotaka, lakini si hilo la kuhusu
mtoto.
"Kila
mtu anajua ipo siku mtoto atakuwa katika hali mbaya na atakuja
kutulaumu sisi, kama ameshindwa kulea mtoto atuletee na si kusema
alibakwa haileti picha nzuri kwa familia yetu."
Sara ambaye sasa anaishi jijini Dar es Salaam anaeleza namna alivyoilea familia hiyo wakati akiishi Igunga.
"Nilimpokea
Shilole akiwa mdogo sana, wakati huo alikuwa akiishi kwa bibi Tatu
ambaye ni ndugu wa mama yake aliyeishi na kaka zake wengine wawili
Kajiwe na Pascal.
Alikuja na kuanza kuishi na mdogo wangu, kwa kuwa nilikuwa mkubwa nilichukua jukumu la kuwalea wote.
Hii ina maana kuwa hajawahi kusoma sekondari kama anavyodai bali alizaa na mdogo wangu baada ya kuishi naye kwa miaka miwili.
"Ugomvi
ulianza kwa kuwa Shilole alikuwa anapenda starehe kuliko mtoto, alitaka
kumwacha mtoto na kumfuata mumewe kwenye starehe wakawa wanabishana
kila siku mpaka alipokutana na dereva wa magari makubwa akatoroka na
kuniachia mtoto akiwa na miezi mitano.
Niliitwa
na mtu na kuambiwa kamchukue shangazi yako kajinyea ndipo nilipomkuta
mtoto ametelekezwa na yeye amekimbia na bwana," anasema Sara.
Anasema
Shilole alirudi Igunga wakati mtoto wake akiwa na umri wa miaka sita.
"Nilimlea mtoto mpaka alipotimiza miaka sita, alirudi Igunga na
kumchukua mpaka mwaka jana alipomleta kunisalimia wakati wa likizo akiwa
na miaka tisa," anasema.
Hata
hivyo, wifi wa Shilole anasema baada ya kumpigia akimtaka ajibu tuhuma
za kubakwa alijibu: "Nimeandika habari zangu za maisha yangu." Kauli
iliyozidi kumfanya ahisi itamharibu mtoto atakapokuwa mkubwa.
Mwandishi wetu alipomtafuta Shilole atoe kauli yake kuhusu suala hilo alisema: "Sina
la kujibu kuhusu hilo kwa kweli na kwa sasa nipo bize sana kwani nipo
katika matayarisho ya filamu mpya hapa."
No comments:
Post a Comment